DODOMA.
SASA ni wazi kwamba serikali mbili zimeonyeshwa taa za kijani baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukamata uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba.
SASA ni wazi kwamba serikali mbili zimeonyeshwa taa za kijani baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukamata uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba.
Jana kamati 14 za Bunge hilo ziliwachagua viongozi
wake; Mwenyekiti na Makamu na 12 kati yake zilichukuliwa na wajumbe
kutoka CCM, chama ambacho tayari kimeweka wazi msimamo wake kuunga mkono
Muungano kuwa ni serikali mbili.
Miongoni mwa waliochaguliwa wenyeviti ni Mbunge wa
Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera
na Uratibu), Steven Wassira na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Ummy Mwalimu ambao wamekuwa mstari wa mbele kupigia chapuo mfumo
huo badala ya serikali tatu zinazopendekezwa kwenye Rasimu ya Katiba.
Wengine ni Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango –
Malecela, Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Job Ndugai, Mbunge wa Viti
Maalumu, Kidawa Khamid Salehe, Mbunge wa Kuteuliwa, Shamsi Vuai Nahodha
na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi.
Wengine wa CCM ni Mbunge wa Viti Maalumu, Anna
Abdallah na aliyewahi kuwa Waziri katika serikali zilizopita Paul
Kimiti. Pia wamo Mbunge wa Wawi ambaye alifukuzwa uanachama na chama
chake cha CUF, Hamad Rashid Mohamed na Mwenyekiti wa kundi la wajumbe
201 wa kuteuliwa na Rais, Francis Michael.
Katika uchaguzi wa Kamati ya Kanuni na Haki za
Bunge, aliyekuwa mwenyekiti wa Muda na Spika wa Baraza la Wawakilishi,
Pandu Ameir Kificho alichaguliwa mwenyekiti na makamu wake, Dk Susan
Kolimba.
Kamati ya Uandishi wa Katiba ilimchagua Mbunge wa
Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na makamu wake, Mgeni Hassan Juma. Kwa
kupata nafasi hizo ni dhahiri kwamba ‘mapishi’ ya uendeshaji wa Bunge
hilo yatafanywa na CCM kwani mwenyekiti wake Samuel Sitta na makamu
mwenyekiti Samia Suluhu Hassan pia ni makada wa chama hicho.
Wenyeviti hao wataungana na Sitta pamoja na Hassan
kuunda Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu, ambayo ndiyo itakuwa na
mamlaka ya kupanga ratiba na miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa Bunge
hilo.
Waliochaguliwa kuwa makamu wenyeviti ni Profesa
Makame Mbarawa, Shamsa Mwangunga, Fatma Mussa Juma, Dk. Sira Ubwa
Mamboya, Assumpter Mshama, Dk. Maua Daftari na Waride Bakar Jabu.
Wengine ni Biubwa Yahya Othaman, William Ngeleja, Salimin Awadh Salimin,
Yusuf Massauni na Thuwayba Kisasi.
Mbowe atimuliwa.
Katika uchaguzi huo, mjumbe wa Bunge hilo, Freeman
Mbowe alitimuliwa katika kamati alikokwenda kushiriki uchaguzi kwa
madai kwamba hakuwa mjumbe.
Mbowe alisema kabla ya uchaguzi huo alimfuata Mwenyekiti Sitta kumwomba wafanye marekebisho katika kamati tatu za Bunge.MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment