DODOMA.
JARIBIO la kutaka kumrejesha bungeni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ili ajibu masuala yaliyoibuliwa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya kufungua Bunge limegonga mwamba.
JARIBIO la kutaka kumrejesha bungeni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ili ajibu masuala yaliyoibuliwa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya kufungua Bunge limegonga mwamba.
Uamuzi wa kukataa ombi hilo ulitolewa jana na
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta wakati akijibu mwongozo ulioombwa
na Mjumbe wa Bunge, Julius Mtatiro, akisema hadhani kama ni sahihi ombi
hilo kutekelezwa.
Awali Mtatiro aliomba mwongozo kwa mwenyekiti,
akitaka kujua iwapo kuna haja ya kumrejesha Jaji Warioba kutoa ufafanuzi
juu ya baadhi ya hoja za Rais Kikwete ambazo zimekinzana na maoni ya
wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.
Mtatiro alisema: “Mtoa hoja mahususi alikuwa ni
Jaji Warioba na Rais Kikwete alialikwa kama mgeni rasmi kufungua Bunge,
lakini badala yake alikuja kujibu hotuba ya Warioba.
“Kwa sababu Rais alikaribishwa kama mgeni rasmi,
lakini alijibu hoja za Warioba, je, hatuoni kama kuna haja ya
kumrejesha mtoa hoja mahususi aje kujenga hoja kutokana na alichosema
Rais Kikwete?” alihoji Mtatiro ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF.
Katika ufafanuzi wake, Sitta alisema tayari
amepokea kwa maandishi kutoka kwa baadhi ya wajumbe kuzungumzia suala
hilo, jambo ambalo litafanyika lakini si kwa kumwita tena Jaji Warioba.
“Tunapenda kupata muda wa kuzungumzia suala hili
ili kuliweka sawa, hotuba zote mbili ambazo ni muhimu zitaandaliwa ili
kupitiwa kuona kama malalamiko yanayotolewa yana hoja,” alisema Sitta.
Tangu Rais Kikwete ahutubie Bunge Ijumaa na kutoa
hoja kinyume na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba, hasa muundo wa
Muungano, kumeibuka mijadala ya ama kuipinga au kuiunga mkono, huku
wengine wakieleza kuwa imekiuka sheria.MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment