
Madrid walipewa penati ya utata muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza lakini Mallenco aliwapa Barcelona penati mbili muda mfupi baadae na kumtoa kwa kadi nyekundu Sergio Ramos ndio maana anaamini refa aliwapendelea Barcelona kwa makusudi.
“Undiano Mallenco hafai kuchezesha michezo ya namna hii, tulikuwa tunacheza dhidi ya wachezaji 11 na mwingine wa ziada, mara zote imekuwa hivi ni kama vile hawataki tushinde ili Barcelona watetee taji la La Liga, sitafuti visingizio lakini sitaki kukaa kimya kuhusu hili, huyu refa hakustahili kuchezesha’
“Nimekuwa hapa kwa muda mrefu wa miaka mitano nafahamu mambo yanavyoenda, kama Barcelona wangepoteza hii mechi wasingekuwa na matumaini ya ubingwa tena, sijawahi kuona Madrid wakipendelewa na refa…. na pamoja na yote yaliyotokea Madrid bado tutachukua ubingwa wa La Liga”
0 comments:
Post a Comment