“Alikutwa (Tuppa) na shinikizo la damu iliyokuwa juu kwa hiyo tulimpokea akiwa mzima.
MARA.
MGANGA Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Marco Nega amesema walimpokea Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa akiwa mahututi na alifariki dakika 25 za matibabu.
MGANGA Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Marco Nega amesema walimpokea Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa akiwa mahututi na alifariki dakika 25 za matibabu.
Dk Nega alisema tayari walikuwa wamejiandaa
kumpatia matibabu, kwa sababu walipewa taarifa mapema kwamba hali yake
ni mbaya baada ya kubadilika ghafla, akipewa taarifa na Mkuu wa Wilaya
ya Tarime, John Henjewele.
Alisema walimpokea Tuppa saa 3:45 asubuhi na
kwamba, baada ya mapokezi walichukua vipimo na kukuta shinikizo la damu
likiwa juu kwa kiwango cha 160/140.
Kwa mujibu wa Mwanasayansi wa Tiba ya Binadamu, Samuel Shita kiwango cha presha cha 160/140mmhg ni shinikizo kali la damu.
Uhatari huo anauelezea ni mbaya zaidi kutokana na namba ya chini 140 ambayo kwa kawaida inapaswa kuwa kati ya 60 na 90.
Dk Nega alisema wakati wakiendelea kujaribu kushusha shinikizo hilo kali, ilipotimu saa 4:15 asubuhi alifariki dunia.
“Tulipigiwa simu kutoka Ofisi ya DC (Mkuu wa
Wilaya) kuwa mkuu wa mkoa analetwa kwa matibabu, tukijiweka tayari kwa
kweli alifikishwa akiwa mahututi hajitambui,” alisema Dk Nega na
kuongeza:
“Alikutwa (Tuppa) na shinikizo la damu iliyokuwa
juu kwa hiyo tulimpokea akiwa mzima…angekuwa amekufa tusingebaini
ugonjwa huo maana mtu aliyekufa vipimo havionyeshi.”
Baadhi ya wajumbe waliokuwa kwenye kikao,
walieleza kuwa mkuu wa mkoa wakati anasomewa taarifa ghafla hali yake
ilibadilika na kuanguka chini na kutokwa na mapovu mdomoni.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama,
alisema Tuppa alikuwa mzima, lakini walishangaa ghafla akiwa amekaa
kwenye kiti alianza kuhema kwa nguvu kabla ya kuishiwa nguvu.
Maiti kuagwa
Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Bendicto ole Kuyan
ametoa ratiba ya awali ya kusafirisha na mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mara, John Tuppa.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment