Raia wa China wanaotuhumiwa kukutwa na pembe za ndovu zaidi ya vipande
700 wakisubiri kuanza kwa shauri lao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory.
DAR ES SALAAM.
RAIA wa China, Huang Gin, Xu Fujie na Chen Jinzha wamedaiwa kutoa hongo ya Sh30.2 milioni kwa polisi na askari wa wanyama pori ili wasipekue nyumba waliyokuwa wakiishi iliyo Mtaa wa Kifaru Mikocheni.
RAIA wa China, Huang Gin, Xu Fujie na Chen Jinzha wamedaiwa kutoa hongo ya Sh30.2 milioni kwa polisi na askari wa wanyama pori ili wasipekue nyumba waliyokuwa wakiishi iliyo Mtaa wa Kifaru Mikocheni.
Washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na nyara za
Serikali ambazo ni vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa
kilogramu 1,880 vyote vikiwa na thamani ya Sh5.4 bilioni.
Shahidi wa upande wa mashtaka, ambaye jina lake
limehifadhiwa kutokana na amri ya Hakimu Isaya Arufani wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Kisutu iliyotolewa jana ya kuvitaka vyombo ya habari
kutotaja majina ya mashahidi watakaotoa ushahidi kwenye kesi hiyo,
alidai kushuhudia tukio hilo.
Alidai kuwa wakati wakiendelea kufanya upekuzi
kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi washtakiwa hao, Huang Gin alivuta droo
na kutoa bahasha iliyokuwa na fedha ndani ambazo walipozihesabu
zilikuwa ni Sh30.2 milioni kama kishawishi cha kuwataka wasiendee
kuipekua nyumba hiyo.
“Hatukukubaliana na ofa hiyo kwa sababu tuliamini
kuna kitu ndani yake na ni lazima tufanye upekuzi na kiasi hicho cha
fedha tukakichukua kama kielelezo cha ushahidi,” alidai shahidi huyo.MWANANCHI.

0 comments:
Post a Comment