CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeweza kujipenyeza katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Kalenga, kikiwa kimefanya mikutano 157 katika kata 13 ndani ya siku 10 tangu kuanza kumnadi mgombea wake, Grace Tendega. Tathmini hiyo ilitolewa jana kwa waandishi wa habari mjini hapa na Mkurugenzi wa Operesheni na Uchaguzi wa CHADEMA, Benson Kigaila, akisema idadi hiyo imefikiwa baada ya mgombea wao kufanya mikutano miwili hadi mitatu kila siku. Kigaila alisema katika mpango kazi wao, walilenga kuzifikia kata zote 13, kazi ambayo wameifanya na kwamba sasa wameshaanza kuingia vijijini ili waweze kuvifikia vyote 71.TANZANIA DAIMA.

0 comments:
Post a Comment