Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Kagera Sugar, Benjamin Effe moja ya michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. |
Akizungumza na Mwanaspoti, Sunzu alisema: “Nasikitika sana kwa matokeo ambayo Simba wanayapata, ni mbaya sana, maskini timu yangu.”
“Kwa nini inakuwa hivyo? Hawana fedha au ni nini? Lakini huenda inachangiwa na kitendo cha kubadili timu kila wakati,” alisema Sunzu.
Simba wikiendi iliyopita ilifungwa mabao 3-2 na JKT Ruvu katika Ligi Kuu Bara huku ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mgambo JKT.
Timu hiyo ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na Mbeya City. SOURCE: MWANASPOTI
0 comments:
Post a Comment