WAJUMBE BUNGE MAALUM LA KATIBA WAPIGWA MKWARA MJINI DODOMA.
Mwenyekiti wa Umoja wa Watumiaji Ardhi ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Maselle Nzingula Maziku (katikati) akitoa tamko la Umoja huo leo mjini Dodoma la kuwataka wanasiasa waliomo katika Bunge hilo kuacha mabishano na badala yake wafanye waliotumwa na wananchi ya kuichambua rasimu ya Katiba ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Wengine katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo ambye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Issa Suleman (kulia) na Kushoto ni Katibu wa Umoja huo na Mjumbe wa Bunge hilo Doreen Maro.(Picha na MAELEZO_Dodoma).
Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba waonywa kuweka mbele maslahi ya taifa
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Peter Kuga Mziray (katikati) akitoa tamko la Kamati ya Uongozi wa Baraza hilo leo mjini Dodoma juu ya mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba ambapo aliwataka kuzingatia kanuni za Bunge hilo zinazokataza vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu ndani ya Bunge. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa Baraza hilo Nancy Mrikaria(kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Siasa wa Baraza hilo Rashid Mtuta (kulia).
0 comments:
Post a Comment