BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA RAIS JAKAYA KIKWETE APIGWA BOMU KATIKA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Mhe. Stephen Masele (MB).

Shinyanga,Tanzania
ASKARI wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania wamemrushia mabomu ya machozi Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele.

Naibu Waziri huyo alipigwa mabomu baada ya kutokea vurugu kubwa katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza FDL kati ya timu ya Stand United ya Shinyanga na timu ya Polisi Mara.Taarifa zinasema kwamba mechi hiyo ilimalzika salama huku wenyeji Stand United wakiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza na Mwandishi wa Habarimpya.com mjini hapa akiwa eneo la tukio Naibu Waziri huyo alisema kwamba vurugu zote zilizosababishwa apigwe mabomu na kuumizwa zilisababishwa na Polisi wenyewe.

"Hizi vurugu zote zimesababishwa na Polisi mpira ulisha malizika na mageti yakafungwa, vijana wote wa Stand United walisha ondoka na kupanda juu ya uwanja kwa nia ya kuondoka uwanjani".

"Lakini chakushangaza Polisi wakawafuata huko na kumkamata mwenzao kisha wanaanza kutupiga mabomu, mimi nafiriki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waangalie mara mbili juu ya ushiriki wa timu nyingi za polisi kwani kila wakati wanabebana na wanapofungwa wanaanza kufanya vurugu" amesema Masele.

Kutokana na vurugu zilizosababishwa na Polisi Uwanjani hapo,kuwa kubwa ndipo walipoamua kurusha mabomu ovyo kwa nia ya kutuliza gasia,huku pia wakirusha mabomu hadi Jukwaa kuu alipokuwa ameketi Naibu Waziri huyo. 


Mbali na Naibu Waziri huyo kupigwa mabomu zaidi ya watu wanne pia walianguka na kuopoteza fahamu baada ya kupigwa mabomu na kukimbizwa Hospitalin ya Mkoa wa Shinyanga kwa matibabu zaidi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: