BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UKAWA HAWAJALIPWA POSHO WASIYOSTAHILI NI BAADA YA KUONDOKA BUNGENI DODOMA.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, viongozi wa Umoja wa Utetezi wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wa Chadema, Freeman Mbowe, wakijadili jambo wakati walipokuwa wakitoka kwenye kikao chao cha umoja huo mjini Dodoma.

DODOMA.  
Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Khamis Hamad amesema wajumbe ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hawajachukua posho wasiyostahili.
Wajumbe hao wamekuwa wakituhumiwa katika mitandao ya kijamii na majadiliano bungeni kuwa wameondoka na posho za Bunge hilo ambazo wamelipwa hadi Aprili 30 mwaka huu.


Wajumbe wa Ukawa waliondoka bungeni Aprili 17 mwaka huu baada ya kulalamikia vitendo vya ubaguzi, matusi na wajumbe kutojadili Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba.


Hamad alisema wajumbe hao walilipwa posho za hadi Aprili 18 mwaka huu. “Tulikuwa tulipe posho za hadi Aprili, lakini baada ya baadhi kuondoka tulibadili utaratibu,” alisema Hamad.


Alisema wanafanya tathmini kujua ni nani wapo ili kuwalipa. “Hata kama mbunge ameondoka akirudi atatuambia, tumlipe fedha yake, lakini sasa tunalipa waliopo bungeni,” alisema na kuongeza:


“Hatuna list (orodha) maalumu ya Ukawa na hakuna mtu aliyetuambia kuwa ameondoka kwa sababu ya Ukawa kwa hiyo watakavyorudi watatuambia.”


Kauli ya Katibu huyo imekuja wakati Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, akitangaza kwamba wajumbe wa kundi la Ukawa hawawezi kulipwa posho kutokana na kususia vikao vya Bunge hilo.


Sitta alitangaza msimamo huo bungeni juzi, akisema hakuna sababu za kuwalipa watu ambao hawajafanya kazi ya Bunge.


Sitta alisema haitakuwa na maana ya wajumbe kulipwa posho, wakati hawajafanya kazi ambayo iliwapeleka Dodoma.


Awali, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima alitoa taarifa kwamba wamekuwa wakishauriana na Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalumu ili kusitisha malipo ya Ukawa.


Malima alisema malipo hufanyika kwa wale wanaokwenda bungeni kwa ajili ya kufanya kazi za Bunge hilo na siyo watu ambao wako nje ya Bunge.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: