BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CDA, BULYANHULU NI JINO KWA JINO KATIKA LIGI YA MABINGWA KITUO CHA MOROGORO.


MSHAMBULIAJI WA KILUVYA UTD, SAID MKINI AKIMTOKA JAMES SALU WA AFRICAN SPORTS KATIKA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA YA MIKOA KITUO CHA MORO.
 


Na Mtanda Blog, Morogoro.
Klabu za Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma na Bulyanhulu FC ya Shinyanga zimeanza kuonyesha dhamira ya kupigana vikumbo kugombea nafasi ya kwanza kituo cha Morogoro katika Ligi ya Mabingwa ya Mikoa kwa kukusanya pointi saba katika ngwe ya kwanza.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka alisema kwa sasa klabu zinazowania nafasi ya kwanza katika kituo hicho ni CDA na Bulyanhulu, ambazo zote zimekusanya pointi saba ila CDA ipo juu kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga baada ya kila timu kucheza michezo mitatu katika michezo 12 ya mzunguko huo.


Abajalo FC ya Dar es Salaam inashika nafasi ya tatu kwa pointi sita baada ya kucheza michezo miwili ikishinda yote, ikifunga mabao sita na nyavu zake zikiguswa mara mbili, wakati African Sports ya Tanga inashika nafasi ya nne kwa pointi tano ikifungwa mabao mawili, kufunga matatu, sare moja na kucheza michezo mitatu.


Mshikamano ya Dar es Salaam yenyewe imekusanya pointi nne katika michezo miwili, ikitoa sare moja na kufunga mabao manne, kufungwa moja na Kariakoo ya Lindi katika nafasi ya sita kwa kuwa na pointi mbili kwa kucheza michezo mitatu ikitoa sare miwili.


Kwa upande wa Kiluvya FC na Navy FC zenyewe zimekusanya pointi moja moja zikifanana kwa kupoteza michezo miwili, kufungwa mabao saba, kufunga matatu, na sare moja, wakati Pachoto Stars ya Newala Mtwara ikishikia mkia kwa kutokuwa na pointi ikipoteza michezo miwili, wakifungwa mabao manne.


Ligi hiyo inaendelea kesho kwa michezo kati ya Mshikamano na Mji Mkuu, huku African Sports ikimenyana na Bulyanhulu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: