BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HABARI YA KUSIKITISHA, MTOTO WA MIAKA 4 AISHI KATIKA BOKSI KWA MIAKA 4 MANISPAA YA MOROGORO.

Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.
Maria Said mama mkubwa wa Nasra, katikati ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box kwa miaka 4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria .
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.


MUME na mke wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box .

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei 20 mwaka huu majira ya saa 4.45 Asubuhi katika eneo la mtaa Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.

Alisema majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria Said na kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika nyumba hiyo na kukuta mtoto huyo akiwa katika box.

Alimtaja mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi minne na nusu ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii ili kuendela nayo.

Afisa Ustawi wa jamii katika ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema mtoto huyo alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu alionekana kuwa na afya dhoofu.

Alisema alilazwa na kwamba kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku wakiwachukulia hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said na Mume wake Mtonga Omari.


Baba mzazi wa mtoto huyo alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.

Alisema kila mara alikuwa akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na hivyo kushindwa kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba alikuwa akimpatia matumizi ya mtoto huyo.


Ofisa mtendaji wa kata hiyo Dia Zongo alisema akiwa katika kazi za kawaida katika Mtaa wa Azimio, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo, alimficha mtoto Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.

Zongo alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kuanza kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa kueleza ukweli juu ya kuwepo kwa mtoto huyo.

Zongo alisema wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah akiwa ndani ya boksi nyuma ya mlango .

Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe, walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha (mtendaji) kutoa taarifa polisi.


Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.


Mtuhumiwa huyo alisema kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana na kwamba alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa limewekwa nyuma ya mlango wa chumba cha mwanamke huyo.

Hores Isaack Msaky Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa matibabu ya awali .

‘’ Tulimfanyia vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema

Alisema bado wanaendela na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.

Alisema mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake pia ni mteke kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia uchunguzi wa kina zaidi.

Baadi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia miaka mine iliopita na kwamba Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo. 




Hata hivyo majirani hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kutokana na kwamba mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na mtoto huyo.http://morondiyohome.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: