BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIVI NDIVYO MLINDA MLANGO WA KLABU YA YANGA SC JUMA KASEJA ALIVYOHITIMU MAFUNZO YA UKOCHA NA KUPATA ALAMA YA DARAJA (A) MOROGORO.


Katibu mkuu wa chama cha soko mkoa wa Morogoro (MRFA) Hamis Semka akimkabidhi cheti mlinda mlango wa klabu ya Yanga, Juma Kaseja baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya ualimu wa mpira wa miguu na kupata alama ya daraja A katika hafla iliyofanyika Bwalo laUmwema la JWTZ Manispaa ya Morogoro, kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Ahmed Mumba.

Na Mtanda Blog, Morogoro.
Mlinda mlango wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Juma Kaseja amehitimu mafunzo ya awali ya ualimu wa mpira wa miguu na kupata alama ya daraja A katika mafunzo yaliyoanza mei 5 mwaka huu katika Manispaa ya Morogoro.


Akizungumza na Mwananchi katika ukumbi wa Bwalo la Umwema la JWTZ mkoani hapa, Mkufunzi wa mafunzo hayo Meja Mstaafu Abdul Mingange alisema kuwa, Juma Kaseja ni miongoni mwa wanafunzi 34 na watatu kati yao wamemaliza kozi hiyo kwa kupata alama ya daraja la A.


Mingange alitaja wengine waliopata daraja A kuwa ni Emmanuel Majengo na Richard Ngwanda baada ya kufanya vizuri katika mitihani ya darasani na vitendo vya uwanjani.


“Juma Kaseja ni wanafunzi wa kozi ya awali ya ualimu wa mpira wa miguu katika mafunzo yaliyoshirikisha wanafunzi 34 na yeye kupata alama ya daraja A ikiwa ni wanafunzi watatu tu waliopata dajala hilo huku 16 wakipata daraja B na watano wakipata daraja C.”alisema Mingange.


Mkufunzi huyo alisema kuwa vitu walivyojifunza katika mafunzo hayo ni pamoja na mpira kinadharia na vitendo, sheria 17 za mchezo wa soka na matibabu ya mwanamichezo ndani ya siku 10 na kuwa mafunzo yalihusisha darasani na uwanjani.


“Kila mwalimu tumempatia DC za kufundishia iwe chini ya mtu ama kuwa na timu ya watoto au wakubwa hilo linategemea pamoja na vitabu vya muongozo wa namna ya kufundisha mchezo wa soka na baada ya miezi sita wanaruhusiwa kuchukua kozi ya mipili ya kujifunza.”alisema Mingange.


JUMA KASEJA.

 
Akizungumzia juu ya kuchukua mafunzo ya kozi ya awali ya ualimu wa soka, Juma Kaseja alisema amekuwa akifanyishwa mazoezi ya soka lakini hakuweza kuelewa ni kwanini anafanyishwa na faida yake lakini kutokana na mafunzo hayo sasa hivi anaelewa kile kinachofundishwa na mwalimu.


Kaseja alisema kwa sasa anajua mambo mengi ikiwemo kupanga program za kufundisha mchezo wa soka huku baadhi ya sheria zingine akizijua akizifahamu na kumpiga chenga hivyo mafunzo hayo yamekuwa na tija kwa kila mshiriki aliyeshiriki.


“Wenzetu wachezaji wa Ulaya jambo hili sio geni sana tofauti na hapa Tanzania, tumeshuhudia Ryan Giggs wa Man United akicheza uwanjani na kufanya kazi ya ukocha hili linafaa kuigwa kwani moja ya faida ya kupata mafunzo ya ukocha huku unacheza ni kufahamu mambo mengi ndani ya soka kwani yataepushwa kufanya makosa yasiyo ya lazima yatayopelekea kuighalimu timi.”alisema Kaseja.


Kaseja alisema kuwa kuhusu mustakabali wa mchezo wa soka baada ya kuhitimu kozi ya awali sio kuacha soka kwa sasa isipokuwa ni kuongeza ujuzi na kuwataka wachezaji wenzake kufanya maamuzi ya haraka ya kupata kozi hiyo ili kumrahisishia mwalimu wakati wa programu zake za kufundisha kwani zitakuwa na faida ya kufahamu kile kinachofundishwa.

“Sina mpango wa kustaafu soka leo wala kesho eti ni kwa sababu nimehitimu mafunzo hayo ya ualimu la haa hasha isipokuwa ni kuongeza ujuzi tu kwani siku za usoni kuna mambo mawili niendelee na soka ama kufanya mambo mengine nje ya soka.”alisema Kasema anayefuata nyayo za Ryan Giggs.

KATIBU WA MRFA.

Naye Mgeni rasmi katika ufungaziji wa mafunzo hiyo Katibu Mkuu wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) Hamis Semka alisema kuwa chama cha makocha nchini (TAFCA) kushawishi wanawake kuchukua mafunzo hayo kwani kwa upande wa wanawake mchezo wa soka upo katika kiwango cha chini na ili kuinua soka la wanawake ni lazima kuzalisha makocha wengi wanawake.

Semka alisema kuwa kwa mkoa wa Morogoro chama chake kipo tayari kuchangia gharama za mafunzo kwa wanawake wataojitokeza katika kozi za soka siku za usoni kwani kuna uhitaji mkubwa wa walimu wa mchezo wa soka kwa wanawake.

“TAFCA jamani jitahidini kuwasawishi wanawake kuchukua mafunzo ya ualimu wa soka hili litasaidia kuinua soka la wanawake hapa Tanzania na hilo chama cha soka mkoa Morogoro tupo tayari kuchangia gharama za mafunzo katika kozi za siku za usoni kwani kuna uhitaji mkubwa wa walimu wa kike wa mchezo wa soka.”alisema Semka.

Semka alisema kuwa TFF na Fifa kwa sasa wanaelekeza katika soka la wanawake mikoani na mkoa wa Morogoro wamefanikiwa kuinua soka kwa upande wa vijana na kuwa na klabu mbili za ligi kuu Tanzania bara Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro SC baada ya mafanikio ya soka la vijana kwa kufanya vizuri katika mashindano ya Copa Coca Cola na Airtel kwa kutwaa kombe hivyo kilichobakia ni kugeukia soka la wanawake.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: