BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KISA CHA MBUNGE WA CCM KUUGUA HAFLA IKIWANI MASAA 36 KABLA YA KUFUNGA HARUSI, HARUSI ILITARAJIWA KUTUMIKA SH96 MILIONI JIJINI DAR ES SALAAM.


Mbunge Vicky Kamata akiwa amelazwa Hospitali ya Tabata General, Dar es Salaam jana. Picha na Florence Majani.

Dodoma/Dar es Salaam.
 

Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.

Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni.


Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.


Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo’ zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.


Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.


“Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia, aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua nilazwe,” alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.


Kamata alifafanua kuwa, pamoja na mambo mengine, hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye kulazwa kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo, haelewi hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati wanaendelea na mipango ya harusi kama ilivyopangwa.


“Mama anaenda nyumbani sasa hivi kuniandalia nguo na kila kitu, lakini sijui itakuwaje kwa sababu daktari amesema kutokana na hali yangu ilivyo, itakuwa vigumu kuvaa viatu virefu na kupata usumbufu wote wa purukushani za harusi,” alisema.


Aliongeza kuwa mipango yote ya harusi ipo tayari kinachosubiriwa na siku yenyewe, lakini kwa bahati mbaya jambo hilo limetokea na haliwezi kuepukika.


Vicky alisema wanakamati wa Dar es Salaam na wale wa Dodoma, wanaendelea na vikao ingawa, wamechanganyikiwa kutokana na sintofahamu iliyopo, kama harusi itafanyika au haitafanyika.


Ndugu wa mbunge huyo akiwemo mama yake mzazi Kamata walionekana hospitalini hapo wakiendelea kumfariji na kujadili kuhusu hatima ya harusi hiyo, iliyokuwa ikingojewa kwa hamu na wanafamilia wote.


Daktari wa Kamata, aliyefahamika kwa jina la Diwani Msemo, alieleza kuwa mbunge huyo alifika hospitalini hapo akiwa na maumivu makali ya tumbo yaliyofanana na uchungu wa kuzaa, hali iliyoonyesha kuwa ujauzito wake unatishia kutoka.MWANANCHI

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: