Mkurugenzi wa Simon Group inayoendesha shirika la Uda.
Dodoma.
Mgogoro wa uwekezaji katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salama (Uda) umechukua sura mpya baada ya Bunge kuamua Mkurugenzi wa Simon Group inayoendesha shirika hilo, Robert Kisena ahojiwe na Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kutokana na kuingilia kati madaraka hayo.
Agizo hilo lilitolewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye alitaka tuhuma zilizotolewa na Kisena dhidi ya Bunge na wabunge zijadiliwe kwa sababu ameingilia uhuru na kinga za Bunge kwa kuzungumza nje ya Bunge masuala ambayo yametolewa maelezo na Serikali bungeni.
Hoja ya Mnyika ilitokana na taarifa za baadhi ya magazeti yaliyotolewa Mei 19, mwaka huu yakimnukuu Kisena akisema kuwa wabunge wa Dar es Salaam wamehongwa na mfanyabiashara mmoja na kwamba kampuni yake inamiliki hisa nyingi tofauti na majibu ya Serikali bungeni.
Akinukuu majibu ya Serikali katika swali lililoulizwa na Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee, Mnyika alisema kuwa Serikali ililieleza Bunge kuwa mgawanyo halali wa hisa za Uda upo kama ulivyosajiliwa kwa msajili wa mashirika ya umma, kwamba shirika hilo linamilikiwa na Serikali na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika kujenga hoja yake Mnyika alisema majibu hayo yalionyesha kuwa Uda ni Shirika la Umma, jambo ambalo lilipingwa na Kisena kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, akisema Uda inamilikiwa na kampuni yake kwa asilimia 76.
Alisema kuwa mwekezaji huyo ameingilia haki, kinga na madaraka ya Bunge kinyume na utaratibu na kuanza kuwatuhumu wabunge ambao walisema ukweli ndani ya Bunge.
Mnyika alisema uhuru wa Bunge wa mawazo umehojiwa nje ya Bunge kinyume cha kanuni, kinga na haki za Bunge jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Bunge.
“Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja na wabunge wenzangu naomba waniunge mkono ili jambo hili liweze kujadiliwa ili Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge imuite na ahojiwe kikamilifu,” alisema Mnyika.
Baada ya hoja hiyo, wabunge wengi walisimama kwa pande zote bila ya kujali itikadi zao za vyama wakiongozwa na wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hata hivyo, Spika Makinda alisimama na kuwataka waketi, ndipo akatangaza kuwa suala hilo haliwezi kujadiliwa bungeni, bali kamati husika itamuita Kisena na kumhoji.
Kisena hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na hata alipopigiwa, simu yake iliita bila ya kupokewa na alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakujibu.MWANANCHI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MKURUGENZI WA SHIRIKA LA USAFIRISHAJI DAR ES SALAAM (Uda) KUJIELEZA MBELE YA KAMATI YA KINGA, HAKI NA MADARAKA YA BUNGE.ieleza bungeni
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment