BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWENGE WA UHURU 2014 WASABABISHA MAHABUSU KUKOSA GARI LA KUPELEKWA MAHAKAMANI MBEYA.

MBOZI-MBEYA. 
Wakati Mwenge wa Uhuru ukizua mvutano mkali bungeni, Dodoma kiasi cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusimama na kutoa ufafanuzi, ujio wa Mwenge huo wilayani Mbozi mkoani, Mbeya umesababisha mahabusi waliokuwa wakisubiri kupelekwa mahakamani jana kukosa gari kwa madai liko kwenye ziara ya Mwenge huo.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Joel Mori alisema mahakamani kuwa sababu za kukwama kwa mahabusi kusomewa mashtaka juzi na jana ni ukosefu wa gari, ambalo kwa sasa linafanya kazi za Mwenge.


“Sababu ni uchache wa magari ya kubeba mahabusi, lililokuwa likitegemewa liko kwenye ziara ya Mwenge iliyoanza Mei 26,” alisema.


Aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza kesi na Hakimu Nemes Chami, alisema kesi hizo zitasikilizwa Juni 9, mwaka huu.


Wabunge Dodoma
Katika kipindi cha maswali na majibu juzi wabunge wa upinzani walisimama wote kupinga mbio za Mwenge kwa madai hazina tija. Juzi, Pinda alitoa ufafanuzi kuwa hakuna dhambi kwa Mwenge kuendelea kukimbizwa nchini kwa kuwa unaimarisha uzalendo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: