BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NI KOSA NCHI YA QATAR KUANDAA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2022 KUTOKANA NA HALI YA HEWA.




Picha ya uwanja utakaojengwa kutumika wakati wa michuano ya 2022.

Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda ulimwenguni, FIFA, Sepp Blatter, amesisitiza ilikuwa kosa kuchagua Quatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022.

Katika mahojiano na televisheni nchini Uswizi, Sepp Blatter aliulizwa iwapo kuiruhusu Quatar kuwa mwenyeji wa kombe hilo ambalo huchezwa kati ya mwezi Juni na Julai ilikuwa kosa, hasa ikizingatiwa kuwa hali ya hewa katika nchi hiyo hufikia hadi nyuzijoto 50 wakati huo.

Alijibu kwa kukiri na kuongeza kuwa kila mtu hukosea maishani. Alipinga madai kwamba taifa hilo lilikuwa limelipia michezo hiyo.

Aliongeza kuwa kamati inayojumuisha maafisa wa FIFA walikuwa wamedhibitisha uwezekano wa taifa hilo kuwa mwenyeji ijapokuwa walikuwa wamepokea taarifa kuhusu vipimo vya juu vya joto.

Alisema kwamba michezo hiyo badala yake inaweza kusogezwa hadi miezi ya mwisho wa mwaka, wakati vipimo vya joto vitakuwa vimepungua.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: