BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

OFISI YA MKAGUZI NA MDHIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (C.I.G) KUANZISHA BENDI YA MUZIKI.









Na Mtanda, Blog Morogoro.
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inatarajia kuunda bendi mpya ya musiki wa dansi kutokana na wafanyakazi wa idara hiyo kuonyesha vipaji lukuki vya kucheza muziki wa aina mbalimbali wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya wafanyakazi wakaguzi wa mapato ya serikali mkoani Morogoro.


Akizungumza na wakaguzi hao hoteli ya Nashera mkoani hapa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh alisema kuwa kutokana na uhodari na vipaji lukuki vya kucheza muziki wa kila aina hivyo ipo haja kwa idara yake kuanzisha bendi ya muziki ili vipaji viweze kutumika katika hafla mbalimba katika taasisi hiyo.

Utouh alisema kuwa baada ya kumalizika mafunzo hayo ya yaliyodumu kwa siku sita alilazimika kuwatengea muda wa wanafanyakazi hao kucheza muziki ndipo alipobaini kuwepo kwa utitiri wa vipaji vya kucheza muziki wa aina mbalimbalo ikiwemo dance, rhumba na bongo flava.


“Hapa leo nataka kuona anapatiakana mshindi wa kucheza muziki kuanzia namba moja hadi tatu na mimi nitatoa zawadi pamoja na meza kuu kwa mshindi wa kwanza sh40,000, wapili sh30,000 na tatu sh20,000 lengo kuona kila mmoja wenu anaondoka Morogoro akiwa na furaha kutokana na kazi ngumu unamzozifanya za kukagua mahesabu.”alisema Utouh.

Washindi wa kwanza, pili na tatu walipatana katika baada ya kushindana kucheza muziki wa aina mbalimbali ambapo Donato Mayo aliibuka nafasi ya kwanza na kujinyakulia kitita cha sh 60,000 wakati Laticia Machibya aliibuka katika nafasi ya pili na kukabidhi sh 30,000 huku nafasi ya tatu ilitwaliwa na Amonon Mwasakatile na kuambulia sh 20,000.

Katika shindano ndogo Lazaro Teobali aliibuka kidedea kwa kuibuka na zawadi ya sh40,000 wakati Agabost Kimath (Papaa) akiambulia sh30,000 wakati Bahati Chilagi akizawadiwa sh30,000 kutokana na kukosa nafasi shindano la kwanza ambapo shindano hilo lilihusisha washindani 13.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: