BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAARIFA KUTOKA DODOMA: MBUNGE WA NKASI ACHAFUA HALI YA HEWA KWA KUWAVAA WANZABAR BUNGENI, HIKI NDICHO KILICHOTOKEA.

 
Mbunge wa Nkasi mh. Ally Kessy asema Wazanzibar Wanachosha, ni Mzigo.
Kutokana na mjadala wa bajeti ya wizara ya mambo ya nje uliokuwa unaendelea , Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy ameporomosha matusi mazito kwa wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao kila mara wanalialia tu kuwa wanabaguliwa , wanadai mambo mengi kuliko uwezo wao na wakati hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama wanaona wanaonewa waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu.

Alienda mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi kwamba ukipigania filimbi wananchi wote wanakusanyika ila bado wanapewa fedha za mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio haki , na pia hata umeme hawalipi na maji pia .


jambo hili lilimfanya mbunge wa CCM ndugu Chombo , kuomba muongozo na Kumtaka naibu Spika a mwambie Kessy kamwe asikanyage Zanzibar , hii ilikuwa baada ya kumuita mwendawazimu , na alisema ni bahati mbaya kwa CCM kuwa na mbunge mwendawazimu kama huyu.

Ndugai muda muda wote alikuwa akicheka , sijui nini maana yake.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: