BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TIMU MBILI ZA SOKA ZAFUZU HATUA YA FAINALI YA KANDA MASHINDANO MAPYA YA CASTLE LAGER PERFFECT 6 2014 MORO.

 Mchezaji wa timu ya soka ya Ndezi FC Delta Thmonas akimpiga chenga Sudi Jabiry wa Nyumbani Park FC kulia wakati wa mchezo wa kusaka timu ya kuchuana na na timu za Dodoma katika ligi ndogo ya mashindano mapya ya Castle Lager Perffect 6 yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro. ambapo katika mchezo huo Nyumbani Park ilitandikwa bao 3-2. PICHA/MTANDA BLOG

Issa Kandula wa timu ya Mzinga FC kushoto akichuana na Twaha Mohamed wa Misufin FC wakati wa mchezo wa kusaka timu ya kuchuana na na timu za Dodoma katika ligi ndogo ya mashindano mapya ya Castle Lager Perffect 6 yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro. katika mchezo huo Mzinga ilifanikiwa kuifunga Misufini kwa bao 3-2.
 
Mchezaji wa Nyumbani Park Jofrey Kautipe kushoto akimtoka mchezaji wa Ndezi FC, Michaael Gadias kulia wakati wa mchezo wa kusaka timu ya kuchuana na na timu za Dodoma katika ligi ndogo ya mashindano mapya ya Castle Lager Perffect 6 yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro. Ndezi ilishinda bao 3-2.

Na Mtanda Blog, Morogoro.
Timu za soka za Mzinga FC na Ndezi FC zimefanikiwa kutinga hatua ya fainali za kanda ya mashariki baada ya kufanya vizuri mashindano mapya ya Castle Lager Perffect 6 yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Ndezi FC na Mzinga FC zimefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kuzifunga Nyumbani Park FC na Misufuni FC kwa idadi sawa ya bao 3-2 katika michezo yao ya fainali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa michezo iliyoshirikisha timu nane mjini hapa, Mwamuzi wa mchezo huo Elly Sasii alisema kuwa ni timu za Mzinga na Ndezi ndizo zilizofanikiwa kutinga hatua ya fainali za kanda ya mashariki ikisubiri washindi wenzao wa mkoa wa Dodoma.

Sasii alisema kuwa Mzinga na Ndezi zitacheza ligi ndogo ya mashindano hayo juni 7 Manispaa ya Morogoro mwaka huu ili kupata timu moja itayowakilisha kanda ya mashiriki katika mashindano ya taifa yatayofanyika baadaye jijini Dar es Saalaam.

“Haya mashindano hapa nchini ni mapya na lengo lake ni kupata timu moja itayoenda Hispania kushuhudia michezo ya Barcelona.”alisema Sasii.

Sasii alifafanua kuwa washindi hayo walifanikiwa kushinda timu nyingine katika hatua ya mtoano, robo fainali ikihusisha timu za Misufini A na B, Nyumbani Park A na B, Airport Rangers na Mtazamo zote za Manispaa ya Morogoro.

Kanda zitakachuana ni pamoja na kanda ya mashariki, Kaskazi, kanda ya Ziwa na kanda za nyanda za juu kusini ambapo baadhi ya kanda michuano hiyo tayari zimeanza rasmi mei 24 mwaka.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: