BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIKIA HAYA YA UKAWA !!! TUSIPOBEMBELEZWA HATURUDI BUNGENI.


Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje akihutubia umati wa wakazi wa jiji la Mwanza kwa tiketi ya Ukawa. Picha na Aidan Mhando.

Na Aidan Mhando, Mwananchi.
Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiwa wanaendelea kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kudai Katiba ya wananchi, bado viongozi hao wanasisitiza kwamba kamwe hawatarudi kwenye Bunge la Malaamu la Katiba kama njia za kistaarabu za kuwaomba warudi hazitatumika.
Kabla ya kuanza kuzunguka mikoani, Ukawa walianza kampeni za kudai Katiba inayotokana na maoni ya wananchi kupitia Bunge Maalumu la Katiba.


Ukawa wanapinga mchakato huo kutekwa na CCM, kwa madai kuwa wamekuwa wakitumia wingi wao ndani ya Bunge hilo kuchakachua maoni yaliyotolewa na wananchi kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Ziara za viongozi hao wa Ukawa mikoani, zina lengo la kuunganisha nguvu za kudai Katiba ya Wananchi na kuwashirikisha wananchi kuhusu kinachofanywa bungeni.


Vyama vinavyounda Ukawa ambavyo viongozi wake wakuu wanazunguka mikoani ni Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena Nyambambe.


Baadhi ya madai ya Ukawa yanayozungumzwa katika ziara hizo ni mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba na kutekwa kwa wanasiasa kutoka chama kilicho na wajumbe wengi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba.


Wakati Ukawa wakiendelea na ratiba zao za kuzunguka mikoani, Bunge Maalumu la Katiba limesimama kwa muda hadi mwezi Agosti kupisha Bunge la Bajeti ambalo linaendelea mjini Dodoma.


Wenje awasha moto Mwanza.
Mbunge wa Nyamagana kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ezekia Wenje, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya fedha ya Ukawa, anasema kuwa hawatarudi kwenye Bunge la Katiba kama njia za kistaarabu hazitatumika kuwaomba warudi.


Wenje alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza katika viwanja vya Dampo mkoani humo.


Akishangiliwa na umati huo wa watu, Wenje anasema Ukawa wataendelea kudai Katiba ya Wananchi hadi pale itakapopatikana. “Kutokana na mapambano yangu bungeni sasa jina limebadilika.



Najulikana Jenero na siyo mtoto wa mama ntilie tena na kwa kudhihirisha hilo nitahakikisha maoni ya wananchi hayachakachuliwi na Katiba itakayopatikana itakuwa ya wananchi wote,” anasema.


“Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) namtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda atumie njia za kistaarabu na kuonyesha ustaarabu katika kutusihi turudi kwenye Bunge Maalumu la Katiba mwezi Agosti la sivyo, hatutarejea ng’o,” anasema.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: