HAWA NDIYO WASHINDI WA TUZO ZA WATU 2014 ZILIZOFANYIKA JANA USIKU JIJINI DAR ES SALAAM.
Mkongwe King Majuto akiwapa mashabiki wake heko kwa kumpigia kura. Ameshinda kipengele cha Muigizaji wa Kiume Anayependwa Kwenye Filamu. Pembeni ni Lulu Michael, mshindi wa Mwigizaji wa Kike Kwenye Filamu Anayependwa.
Mtangazaji maarufu Salim Kikeke wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ametwaa taji la Mtangazaji wa Runinga Anayependwa katika toleo la kwanza la Tuzo za Watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards katika sherehe zilizofanyika Serena Hotel, Ijumaa jijini Dar Es Salaam.
Vipengele 11 (kumi na kimoja) vilikuwa vikishindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na tuzo. Chini ya orodha ni picha za tukio hilo.
ORODHA YA WASHINDI
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
Millard Ayo – Clouds FM
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
Amplifaya – Clouds FM
3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
Mkasi – EATV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
Juma Kaseja – Yanga
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
Nisher
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
My Number One – Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
Yahaya – Lady Jaydee
09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
King Majuto
10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU INAYOPENDWA
Ndoa Yangu
Salim Kikeke wa BBC Dira ya Dunia, mshindi wa kipengele cha Mtangazaji wa Runinga Anayependwa, akizungumza machache baada ya kutangazwa.
Picha ya pamoja ya walionufaika katika Tuzo za Watu mjini Dar Es Salaam, Juni 27, 2014.
Hamza Kasongo, mkongwe katika fani ya utangazaji Tanzania akimkabidhi Tuzo Salim Kikeke.
Luca Neghesti na Nancy Sumari waandaaji wa shughuli ya Tuzo za Watu. Wao pia wanahusika na Bongo5.com.
Salim Kikeke (katikati), Mtangazaji wa Runinga Anayependwa akiwa na Luca Neghesti na Nancy Sumari waandalizi wa Tuzo za Watu. MC Jimmy Kabwe akiwa kazini – Tuzo za Watu 2014.
Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lynn
Faraja Nyalandu
Salim Kikeke wa BBC, Mzee wa Dira ya Dunia TV.
Jacqueline Wolper naye alikuwepo.
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
Kichwa chenyewe ndiyo hiki, Luca Neghesti mwasisi wa Tuzo za Watu. Kijana ana mipango mizuri, anastahili kuungwa mkono. Boss wa Bongo5 pia.
Millard Ayo wa Clouds FM akifika kuchukua tuzo yake.
Mutu ya Kilo, JB
JB akimkabidhi Lulu Michael tuzo ya Mwigizaji wa Filamu wa Kike Anayependwa.
Sasa hapa Majuto (kofia nyeupe) huwezi kujua anaigiza au la! Lakini huyu kweli mkongwe, toka enzi za DDC Magomeni Kondoa, chuma kimedumu sana hiki. Jacqueline Wolper yuko na simu, sijui ni Instagram au…!?
Kwa warembo hawa, hapa King Majuto lazima kaongezeka umri.
0 comments:
Post a Comment