BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BUGURUNI NI NOMA SANA YAANI NDANI SAA 2 USIKU NI HATARI KWA KUPITA ENEO HILO JIJINI DAR ES SALAAM.


Buguruni ni jina la kata ya Ilala katika Dar es Salaam. Ilala yenyewe inahesabiwa kama manispaa ya Ilala ndani ya jiji la Dar es Salaam. Inajumlisha kitovu cha kihistoria cha Dar es Salaam ambako kuna ofisi nyingi za serikali pamoja na kampuni na maduka. Nafasi ya kitovu chenyewe ni sanamu ya askari; mitaa mingine maarufu ni Kariakoo, Buguruni na Kivukoni.


Dar es Salaam. “Naombeni msaada…Wananipiga jamani…Tafadhari ndugu zangu niokoeni wataniuwa mimi,”…Ni sauti ya kijana anayepigwa na kundi la vijana kutokana na tuhuma za wizi eneo la Buguruni majira ya saa moja na nusu usiku.


Vijana hao wanaonekana wenye hasira kali na jazba bila ya kujali malalamiko ya mwenzao wanaendeleza kipigo. Wakati kijana huyo anaendelea kupokea kipigo kutoka kwa vijana hao walioukuwa wanamvuta pembeni mwa barabara sambamba na kumchania shati lake, vijana wengine watatu wanajitokeza na kuungana nao kuendeleza kipigo.


Ni jambo la kushangaza, hata wakati tukio hilo linaendelea hakuna mpita njia mwingine aliyeonyesha kuguswa zaidi ya vijana hao watatu.


Pilikapilika za watu katika eneo hilo zinaendelea kama kawaida.Wengi wakiwa wanarejea katika shughuli zao mbalimbali za kujitafuatia riziki za kila siku na wengine wanaendelea na biashara.


Kumbe katika harakati hizo za wengine kurejea nyumbani baada ya kazi za siku, kuna wengine kwao ndiyo muda wa kutafuta riziki.Kutafuta riziki huko kupo kwa namna tofauti tofauti. Kuna wale wanatafuta kwa njia za hali na zile zisizo za halali ilihali tu mwisho wa siku mkono uende kinywani bila ya kutiwa mikononi wa polisi wala wananachi wenye hasira kali.


Tukizungumzia wale wanaotafuta riziki kwa njia zisizo za alali tunamaansha watu wanaojihusha na wizi, uporaji, utapeli, uporaji na kujiuza kwa maana ya kahaba.


Ujanja wa waporaji wa Buguruni
Wizi hasa wa mifukoni na kwenye mikoba hasa kwa kinamama umezoeleka sana katika maeneo mengi yenye msongamano wa watu. Ukizungumzia kwa wanawake juu ya suala hili basi kila mmoja anaweza kukupa stori yake lakini kwa Buguruni hali ni tofauti.


Wezi wa eneo hilo hutumia mbinu tofauti ambazo hazijazoeleka sana na vibaka wengine. Ukiwa mgeni wa eneo hili na kama hufahamu vizuri jiografia ya hapo basi unaweza kuibiwa bila la kujitambua.


Kutokana na hali ya watu kuwa wengi na pilikapilika nyingine vibaka hutumia mwanya huo kutimiza malengo yao japo kwa upande wao ni kujipatia riziki, lakini kwa njia isiyo halali.


Kwa muda wa kama saa takriban mbili mwandishi wa gazeti hilo alipokuwa katika eneo hilo akishuhudia baadhi ya vijana ambao huwa wanadaiwa kutembea kwa makundi nakujifanya kuwa wanagombana, lakini ugomvi huwa machoni mwa watu wengine na wao wakiwa wamepanga njama ya kuiba.


Siku hiyo kama bahati kwa gazeti hili, lilishuhudia wakiwa kwenye harakati za kufanya tukio la wizi, kwani kwa wazoefu wa eneo hilo wanasema vijana hao hutumia mbinu hiyo mara chache ili watu wasiizoe.


Kundi hilo la vijana wapatao kumi hivi walitokea upande wa Barabara ya Mandela kuanzia Buguruni hadi Tazara, wakiwa wanazozana na kutupiana ngumi wengine wakiwa wanajifanya kama wanajaribu kuamua ugomvi. Wakaendelea kuvutana hadi Tazara kuelekea kwenye kituo cha daladala eneo hilo.


Mzunguko wa aina hiyo hufanywa kwa pande zote nne kwa maana ya upande wa kituo cha daladala cha kuelekea Tazara, Ubungo na Posta.


Kwa wazoefu wa eneo hili hasa wafanyabiashara ndogondogo wanauza bidhaa mbalimbali tabia hiyo sito ngeni kwao. Hivyo wao walionekana kutojali na kuendelea na shughuli zao, kuhudumia wateja wao bila kutilia maanani ya kilie kilichokuwa kinajiri kwa wakati ule.


Pia kwa wapitanjia na watu ambao siyo wazoefu wa eneo hili walibaki wameduwaa, wengine wakitamani kuingilia kati kuamua ugomvi wa vijana hao waliokuwa wanapigana.


Katika kutaka kudadisi ili kujua hasa ni nini kilikuwa kinaendelea, alidokezwa kuwa ugomvi ule ni mbinu ya vijana hao kutaka kuiba na kupora vitu vya watu.


Wakati wanavutana vile na kutupiana ngumi ndani ya lile kundi unakuta wameshamwibia mtu, sasa ili kuondoa wasiwasi kwa watu wanafanya hilo ili wasitambulike na wakifika kituoni tena kwa wale watakaokuwa wanashangaa, pia watakacho kutananacho ni halali yao.


Mathalan, jambo la kushangaza za zaidi ni kwa jinsi vijana hao wasivyo na tone la huruma kwa wale wasamaria wema wasiojuwa mbinu hiyo, ambapo wakijaribu kuamua ugomvi huo hujumuishwa kwenye kundi hilo na kugeuzwa mwizi na kumpora kila kitu alichokuwa nacho.


Pia, gazeti hili lilishuhudia abiria walioukuwa wanasubiri daladala kituoni hapo wakinyakuliwa baadhi ya vitu vyao na vibaka ambao wanajificha kwa miamvuli ya wapigadebe.


Kwa upande wa wizi huu hawa jamaa wanakuwa na utu kidogo. Japo kwa abiria ambao ni wazoefu huwa wanajihami hasa wanawake.Kinamama wengi wanapokuwa katika eneo hili hujitahidi kushika mikoba yao kwa umakini wa hali ya juu.


Wale wanaobeba mabegi ya mgongoni kwa ajili ya kompyuta mpakato (laptop), huwa wanageuza ubebaji wake na kuyabeba mbele kwa maana ya kifuani badala ya mgongoni ili kuhakikisha usalama wa mali zao.


Licha ya jitihada zote hizo za kujihami wanazofanya abiria, bado hawa jamaa wamekuwa wakifanikiwa kupora watu mali zao zikiwamo simu za mkononi na fedha.


Gazeti hili lilishuhudia jinsi ambavyo jamaa mmoja alinusurika kupoteza vitambulisho vyake baada ya kibaka mmoja kumwibia baada ya kwenda pembeni na kugundua siyo hela alirejesha na kutoa matusi kwa hasira.


Ilikuwa hivi, abiria huyo alikuwa miongoni mwa abiri wengi waliokuwa wanasubiri usafiri katika kituo hicho. Baada ya daladala tofauti kupita kituoni hapo ikaja daladala moja iliyokuwa imetoka Ubungo kuelekea Temeke, bila shaka alikuwa anasubiri usafiri huo uliomchukua yeye na abiria wengine muda kufika kituoni ikiwa na nafasi ya wao kupanda.


Kutokana na kuwawepo abiria wengine ndani ya daladala ile, ilimlazimu abiria huyo pamoja na wenzake kugombania usafiri huo kwa nguvu kama ilivyozoeleka kwa usafiri wa daladala hasa majira ya jioni na asubuhi.


Katika harakati hizo kuliwa na abiria na wale majamaa waliozoeleka kuwa ni wapiga debe, lakini kumbe wengi wao ni vibaka.Wakati wa kupanda daladala baadhi hujifanya kuendelea kupiga debe na wengine wakijumuika na abiria kupanda daladala. Ndivyo ilivyokuwa hapo.


Bila ya kufahamu hili wala lile jamaa akawa anagombea kuingia kwenye daladala mmoja wa vibaka hao wakiwa ameshachora ramani ya kumwibia. Wakati wa purukushani hizo yule kikaba alifanikiwa kumchomolea kitu ambacho alidhani ni hela.


Kwa kuwa nia yake ilikuwa ni kuingia ndani ya daladala hakuwa na wasiwasi wowote hivyo hata hakujitizama ndani ya mifuko yake. Akasimama akisubiri daladala ianze safari yake. Jambo la kushangaza ni wakati ile daladala imesimama kusubiri magari yaliyokuwa yamesimama mbele yake kutokana foleni yasogee, yule kibaka alirejeja na kurusha vile vitambulisho ndani ya daladala na akitoa matusi na kufyonza.


Hali hiyo iliwapelekea abiria wa daladala kila mmoja kutahamaki.Kila mmoja alianza ‘kujisachi’ ndani na mifuko na mikoba kwa upande wa wanawake. Ndipo yule jamaa akagundua kuwa alikuwa ameibiwa vitambulisho vyake na kuviokota.


Abiria mwingine wa kike naye aligundua kuwa mkoba wake ulikuwa umeanza kuchanwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali mithili ya wembe na kuanza kutoa matusi ya kumtukana aliyejaribu kufanya kitendo hicho.


Hata hivyo, inadaiwa kuwa kundi hilo ni kubwa hivyo mtu akijaribu kumdhuru mmoja wao hupanga njama ya kulipa kisasi kwa yeyote aliyehusika na jambo hilo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: