MARADHI YA EBOLA YAUA DK UMAR KHAN SIERRA LEONE.
Daktari mwenye umri wa miaka 39 aliyekuwa akiongoza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola huko Sierra Leonne amefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
Mganga mkuu wa nchi hiyo anasema Dr.Umar Khan alifariki dunia Jumanne jioni.
Kifo cha Khan kimetokea wiki moja tu baada ya kugunduliwa na ugonjwa huo, na kutangazwa siku ile, ile rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma alikuwa anatarajiwa kutembelea kituo cha matibabu ya wagonjwa wa Ebola cha mji wa kaskazini mashariki wa Kailahun.
Kijana huyu daktari ambaye ametibu zaidi ya watu 100 wenye ugonjwa wa Ebola alikuwa ni shujaa wa taifa huko Sierra Leonne.
0 comments:
Post a Comment