BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MCHAKATO WA KATIBA MPYA !!!: NAIBU KATIBU MKUU CCM TANZANIA BARA HIVI NDIVYO ANAVYOWABEMBELEZA VIONGOZI WA UKAWA KURUDI BUNGENI.


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM bara), Mwigulu Nchemba.

Mwanza/Dar es Salaam.
 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM bara), Mwigulu Nchemba ameutaka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kurejea bungeni ili kukamilisha Mchakato wa Katiba Mpya kwa amani na utulivu.


Rai hiyo imekuja wakati mijadala mbalimbali inaendelea juu ya hatima ya wajumbe hao na mchakato huo tangu walipotoka bungeni na kususia vikao vya Bunge hilo Aprili 17 na kukataa kurejea, huku zikiwa zimesalia siku tisa kabla ya Bunge hilo kuendelea na vikao vyake mjini Dodoma Agosti 5.


Akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho mjini Mwanza jana, Nchemba alisema:“Natoa rai kwa wenzetu…turudi ili tupate majibu ambayo ni Katiba Mpya. Tuachane na haya mambo.”


Naibu huyo alisema: “Huu ndiyo wakati wa kutengeneza Katiba ambayo itakuwa Sheria mama itakayotumika kwa miaka 50 ijayo, hivyo wajumbe hao lazima wazingatie jambo hilo.”


“Halafu wanasema tuache..kwa nini tuache wakati hatujafikia sehemu ya kujadili mambo yanayowahusu Watanzania,” aliohoji Nchemba.


Alisema kuwa, badala ya kuendelea na mgomo huo ni vyema wajumbe hao wangeweka wazi nia yao tangu machakato huo ulipoanza kuliko mambo wanayoyafanya sasa huku gharama nyingi zikiwa zimeshaumika kwa ajili ya kuendesha mchakato wa Katiba Mpya.


“Tumeshatumia fedha nyingi, zaidi ya Sh7 bilioni pamoja na zile zilizotegwa ili kukamilisha mchatako huu wa siku 130 za shughuli hizo. Ikumbukwe kuwa fedha hizo ni kodi za Watanzania ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu mchako umalizike ili wapate Katiba wanayoitaka,” alisema.MWANANCHI

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: