BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIA WA KIPALESTINA SASA WAKIMBIA MJI WA GAZA KASKAZINI, KISA MAKOMBORA YA ISRAEL KUELENGA MJI HUO.

Wapalestina wahama Gaza kaskazini
Mamia ya Wapalestina wamekuwa wakikimbia sehemu za kaskazini za Gaza, baada ya Israel kuonya kuwa italenga sehemu hiyo katika mashambulio yake ya sasa.

Umoja wa Mataifa umenukuliwa ukisema kuwa watu kama 4,000 tayari wameomba hifadhi katika hifadhi ya muda.

Jumamosi usiku mashambulio ya ndege za Israel yaliendelea Gaza.

Wapalestina zaidi ya 160 wameuwawa hadi sasa.

Hamas imerusha makombora zaidi dhidi ya miji ya Israel pamoja na Tel Aviv; hakuna mtu aliyekufa Israel.

Israil ilisema wanajeshi wane walijeruhiwa waliposhambulia eneo ambapo makombora yakirushwa.

Hamas inasema wanajeshi wa Israil hawakuwahi kufika ardhini.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: