BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAASISI YA WANAWAKE WA KIISLAM TANZANIA YAMWAGA MISAADA KEDEKEDE KWA WATOTO YATIMA KIJIJI CHA MAGOLE WILAYANI KILOSA MOROGORO.


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (TAQWA), Dk Salha Kassim kulia akizungumza jambo na mtoto Sheila Salehe (13) akimkabidhi mfuko wa unga wa sembe na mafuta ya kula wakati wa utoaji wa sadaka ya mwezi wa ramadhani kwa watoto yatima msikiti mkuu wa ijumaa wa kijiji cha Magole wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ambapo watoto yatima 98 walikabidhiwa msaada wa chakula wenye thamani ya sh 3 milioni. Kushoto ni mkurugenzi wa watoto katika jumuiya hiyo, Kamaria Kimeza.PICHA/MTANDA BLOG











 
Baadhi ya walezi na ndugu wa watoto yatima katika kijiji cha Magole wakiwa na viroba vyenye vyakula baada ya Taasisi ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (TAQWA) kutoa msaada kwa watoto yatima 98 wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro ambapo watoto yatima 98 walikabidhiwa msaada wa chakula wenye thamani ya sh 3 milioni.
 
Na Mtanda Blog, Morogoro.
Taasisi ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (TAQWA) wametoa msaada wa chakula kwa watoto yatima zaidi ya 98 wa kijiji cha Magole wenye thamani ya sh 3 milioni katika Wilaya ya Mvomero.

Pamoja na tatizo la upungufu wa chakula lakini pia watoto hao wanakabiliwa na changamoto ya kutopata elimu stahiki.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Katibu mkuu wa msikiti mkuu wa Ijumaa Magole uliopo wilaya ya Kilosa, Athman Mparo alisema kuwa jumla ya watoto yatima 98 wa kijiji hicho wanakabiliwa na changamoto ya kupata elimu duni hasa baada ya sensa iliyoibuliwa na jumuiya ya wanawake ya kutaka kutoa sadaka kwa watoto yatima wa kiislama katika kipindi cha mwezi mkutukufu wa ramadhani.

Mparo alisema kuwa yatima hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wengi wao kukosa elimu ya msingi, chakula cha kutosha, kutoka kwa walezi wao ama ndugu zao kutokana na kushindwa kuwahudumia kama watoto wengine kwani wengi wao kupotelewa na vifaa vya shule kutokana na mafuriko yaliyoikumba kijiji hicho januari 21 mwaka huu.

“Uongozi wa hii Taasisi ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania ilikuja na masharti ya kupata watoto yatima wa kiislamu waliofiwa na baba yao wenye chini ya umri wa miaka 18 na wale waliozaliwa ndani ya ndoa ila nasi katika sensa yetu ya kusaka yatima hao tukagundua kumbe wanachangamoto pia ya kukosa elimu ya msingi.”alisema Mparo.

Alisema kuwa katika sensa hiyo iligundulika kuwa kuna yatima 98 wa kiislam na kati ya hao wanaosoma ni 44 ikihusisha shule ya msingi 35 na sekondari tisa huku 54 wakikosa elimu.

Msaada huo uliotolewa na Taasisi hiyo ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (TAQWA) ni sehemu ya sadaka ya mwezi mkutukufu wa ramadhani mkoani Morogoro.

Akizungumza na walezi na ndugu wa watoto hao katika msikiti mkuu wa Ijumaa wa Magole Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (TAQWA), Dk Salha Kassim alisema kuwa jumuiya yao imetoa msaada ya chakula kwa watoto yatima 98 katika kijiji cha Magole ilikiwa sehemu ya majukumu makuu ya kuwawezesha watoto baada ya kufanyika kwa  sensa.

Vyakula vilivyotolewa ni pamoja na mchele kilo 10, sembe kilo tano, maharage kilo tatu, sukari kilo tano, ngano kilo tano, mafuta ya kula lita tatu, chumvi na na tende pakti moja moja.

“Jumuiya yetu ya Taqwa mpaka sasa tayari tumeshatoa msaada kwa watoto yatima katika mikoa ya Pwani-Bagamoyo, Zanzibar-Pemba, Magole-Morogoro, na Dar es Salaam ambako kwa Dar es Salaam kila mwezi watoto zaidi ya 70 hupatiwa mahitaji muhimu na jumuiya hii.”Dk Salha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: