Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka "hatua za dharura" zichukuliwe
ili kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Africa magharibi, ambao
umewauwa zaidi ya watu 400. Ugonjwa huu ndio mkubwa zaidi duniani kuzuka
kutokana na visa vyake, vifo na kusambaa katika maeneo.
Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres (MSF) tayari limeonya
kuwa kusambaa kwa ebola hakuwezi kudhibitiwa. Shirika hilo lina
wafanyikazi 300 wa kimataifa na vile vile wa kitaifa wanaofanya kazi
nchini Guinea, Sierra Leone pamoja na Liberia, ambako ugonjwa huo
unaenea kwa kasi. Mataifa mengine yako macho iwapo ugonjwa huo utasambaa
Zaidi.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Ebola ni ugonjwa unaosababishwa
na virusi na ambao dalili zake za mwanzo huweza kuwa kushikwa na homa,
kuwa dhaifu, kuumwa na misuli na kuumwa na koo. Na huo ni mwanzo tu:
kile kinachofuata ni kutapika, kuendesha na -wakati mwingine- kuvuja
damu.
Virusi hivyo huenea kwa haraka sana, na hadi sasa hakuna dawa
inayotambulika kuweza kuvitibu, kwa hivyo wanaotoa huduma za matibabu
huvalia mavazi yanayowakinga kutokana na kuambukizwa kwa ugonjwa huo.
Kulingana na uzito wa athari za ugonjwa huo, hadi kufikia asilimia 90 ya
walioambukizwa huaga dunia. Anayehakikisha usafi anawakaribia wagonjwa
wanaosubiri matokeo baada ya kupimwa damu.
Vipimo vya maabara vitaonyesha kwa saa kadhaa iwapo sampuli ya damu inayopimwa ina virusi vya Ebola au la.
Baada ya kukumbana na virusi hivyo katika sehemu iliyotengwa, mavazi na viatu husafishwa kwa Chlorine.PICHA/BBC

0 comments:
Post a Comment