BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UNYANYASAJI KWA WATOTO BADO WAITESA MOROGORO, MTOTO MUNGINE ALAZWA UVUNGU WA KITANDA KWA MIAKA TANO ILI MAMA MZAZI APATE NAFASI YA KUUZA POMBE ZA KIENYEJI KILABUNI DUMILA-KILOSA.

Devotha akiwa amelazwa katika chumba maalum hospitali ya mkoa wa Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.

Devotha akichunguzwa afya na daktari hospitali ya mkoa wa Morogoro baada kupokelewa kutoka hospitali ya wilaya ya Kilosa.PICHA/MTANDA BLOG.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akimjulia hali mtoto huyo.PICHA/MTANDA BLOG.

MTOTO ALIYEFICHWA UVUNGUNI MWA KITANDA, AFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA, ABAINIKA KUWA NA UTAPIAMLO, MARALIA NA UPUNGUFU WA DAMU MORO.
Hamida Shariff, Morogoro.
Morogoro... Uchunguzi wa awali wa afya ya mtoto Devota Malole (7) aliyefichwa ndani ya mvungu wa kitanda kwa miaka mitano na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Sarah Mazengo imebainika kuwa mtoto huyo ana utapiamlo mkali, maralia na upungufu wa damu.


Taarifa za ukatili wa mtoto huyo mwenye mlemavu wa viungo na akili zilitolewa Julai 10 mwaka huu na viongozi wa kijiji cha Matongola tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa ambapo baadaye alipelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Kilosa ambako alifanyiwa uchunguzi na kubaini magonjwa hayo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kabla mtoto huyo kuhamishiwa katika hospitali ya rufaa Mganga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya aya Kilosa Dkt. Frank Kimoleta alisema kuwa pia mtoto huyo anamajeraha makubwa sehemu ya makalio yaliyotokana na kulazwa chini kwa muda mrefu.

Dkt. Kimoleta alisema kuwa pamoja na kufanyiwa vipimo hivyo lakini pia mtoto huyo anahitajika kufanyiwa uchunguzi wa kina kuhusu afya yake na pia anatakiwa kuwa karibu na uangalizi wa madaktari ili kufuatilia afya yake wakati wote.

Wiki iliyopita mtoto huyo alihamishiwa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro akitokea wilayani Kilosa na baada ya kufikishwa hospitalini hapo alilazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu ICU na madaktari wanaendelea kuchunguza zaidi afya yake.

Uchunguzi uliofanywa na mwanadishi wa habari hizi ulibaini kuwa Sarah Mazengo ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo ni mfanyabiashara wa pombe za kienyeji na alikuwa akimfungia ndani mtoto huyo wakati na kwenda kilabuni kuuza pombe.

Naye afisa ustawi wa jamii mkoa wa Morogoro Oswin Ngungamtitu alisema amesikitishwa sana na kitendo alichofanyiwa mtoto huyo kwani ni ukiukwaji wa haki za watoto wenye ulemavu na kwamba ofisi yake itahakikisha mtoto huyo anapatiwa matibabu ya magonjwa yatakayobainika.

“Hata miezi miwili bado tangu tukio la mateso yaliyosababisha kifo Mtoto Nasra Mvungi kuripotiwa, lakini bado jamii imekuwa ikiendelea na vitendo vya ukatili na mateso kwa watoto na baya zaidi watoto wanaofanyiwa vitendo hivi ni walemavu, nawaomba wananchi tushirikiane kuwafichua watoto hawa,” alisema Ngungamtitu.

Polisi mkoani hapa Leonard Paulo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

MBUNGE ALAANI KITENDO CHA MTOTO KUFICHWA UVUNGUNI MWA KITANDA.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini AbdulaAziz Abood amelaani kitendo cha kuteswa na kufanyiwa ukatili mtoto Devota Malole (7) aliyefichwa ndani ya mvungu wa kitanda kwa miaka mitano na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Sarah Mazengo.

Akizungumza mara baada ya kufika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro na kuona hali ya mtoto huyo Abood aliviomba vyombo vya sheria kuchunguza kwa kina chanzo cha matukio ya aina hii na kutoa adhabu kali kwa watakaopatikana na hatia kwa vitendo hivyo.

Aidha Abood alisema kuwa kutelekzwa na waume zao isiwe sababu ya wanawake kutesa na kufanya ukatili kwa watoto kwani zipo idara zinazosaidia wanawake waliotelekezewa familia.

Alisema kuwa hata yeye binafsi kama Kiongozi yuko tayari kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo walemavu hivyo aliwataka wanawake kuacha tabia ya kuwafanyia ukatili watoto ambao wana haki ya kuishi hata kama ni walemavu.

“Jamii bado haijasahau mateso aliyoyapata mtoto Nasrah na kusababisha kifo chake, hivi karibuni tena linatokea tukio jingine kwa kweli hii ni aibu kwa mkoa wa Morogoro na mpaka sasa haijafahamika chanzo cha matukio haya hasa ni nini,” alisema Abood.

Alisema kuwa atawasiliana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera ili kuangalia namna ya kutoa matamko kutokana na matukio haya na wakuu wa Wilaya watahusika katika kusimamia matamko hayo.

Aliiomba jamii kuendelea kuwafichua watoto wanaopata mateso na ukatili katika maeneo yao na kwamba yeye kama mbunge atafuatilia kwa karibu huduma na matibabu ya mtoto Devota Malole kwa wakati wote atakapokuwepo hospitalini hapo.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Alsaed, Omary Alsaed alihaidi kugharamia matibabu ya mtoto huyo pamoja na mahitaji mengine na hata akihitajika kwenda kutibiwa nje wa nchini ameahidi kumsafirisha kwa gharama zake.


Alisema kuwa ameguswa na hali ya afya ya mtoto huyo na kwamba aliahidi kutoa zawadi nono kwa mtu atakayefichua vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hasa wenye ulemavu.CHANZO/MTANDA BLOG.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: