BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWENYEKITI WA CHADEMA KUWABEBA NA KUWAPELEKA MASHAHIDI KATIKA KESI YA KUMSHAMBULIA MWANGALIZI WA UCHAGUZI MWAKA 2010 MAHAKAMA YA WILAYA.


Upande wa utetezi katika kesi ya tuhuma za kumshambulia mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, utawasilisha mahakamani orodha ya mashahidi wake leo.


Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema) na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, anatuhumiwa kumshambulia Nassir Yamin, ambaye alikuwa ni mwangalizi wa ndani katika uchaguzi huo. Kesi hiyo imepangwa kutajwa leo katika Mahakama ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Amri kutakiwa kuwasilisha mahakamani orodha ya mashahidi wake, unatokana na uamuzi uliotolewa hivi karibuni na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Denis Mpelembwa.

Katika uamuzi wake, Hakimu Mpelembwa alisema Mbowe ana kesi ya kujibu katika shitaka la kumshambulia mwangalizi huyo wa ndani. hivyo, mahakama hiyo ilisema kuwa mashahidi saba wa upande wa mashtaka tayari wamefanikiwa kuishawishi kwamba, siku ya tukio hilo kulikuwa na tafrani iliyojitokeza na kwamba, kwa mantiki hiyo, Mbowe atatakiwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na tuhuma za kuhusika kwake.

Ingawa upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Albert Msando na Issa Rajabu ulitoa hoja mahakamani hapo kwamba, ushahidi wa Jamhuri uliacha mashimo mengi, Hakimu Mpelembwa anaona Mbowe ana kesi ya kujibu.

Hata hivyo, katika uchaguzi huo, Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM) aliyepata kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) kura 258 na Petro Kisimbo (TLP) kura 135.


CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: