Kiungo mshambuliaji wa timu ya Kihonda Magolofani, Andendekisye Mwalupanga kushoto akiwania mpira dhidi ya mlinzi wa Msamvu Terminal FC, Aloyce Mwakatobe wakati wa ligi ya kugombea jezi iliyofikia hatua ya robo fainali katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.
PICHA/MTANDA BLOG.
Klabu ya soka ya Burkina FC ya mkoa wa Morogoro ipo katika mandaalizi makali ya kujiwinda na ligi daraja la kwanza kwa msimu wa mwaka 2014/2015 inayotarajia kutimua vumbi oktoba 4 mwaka huu katika uwanja wao wa shule ya msingi Mafisa mkoani hapa.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mjini hapa Kocha mkuu wa klabu hiyo, Charles Mwakambaya alisema kuwa klabu tayari imeanza mapema maandalizi ya ligi daraja la kwanza kwa ajili ya msimu wa mwaka 2014/2015.
Mwakambaya alisema kuwa maandalizi hayo wameanza mapema ili kuwapa fursa wachezaji wapya kuzoena na wenzao baada ya kusajili wachezaji 12 ambao wameungana na wachezaji wa zamani 13, lengi likiwa kuzoana na kutengeneza timu imara na yenye ushindani katika ligi hiyo.
“Tumeanza maandalizi mapema kwa sababu tuna wachezaji 12 wapya ambao wameungana na wenzao wa zamani 13 na lengo letu ni kutengeneza timu imara yenye ushindani kuanzia safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji ili kupata ushindi na kutimiza ndoto yetu ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa ujao.”alisema Mwakambaya.
Mwakambaya alifafanua kuwa achilia mbali kusajili wachezaji hao 12 kati yao wachezaji wanne wamepandishwa kutoka timu B na kuwa wachezaji wengine wamesajiliwa katika timu mbalimbali.
Mwakambaya alisema kuwa baada ya kikosi chake kuzoena watacheza mechi za kujipima nguvu michezo nane, sita ikihusisha timu za mkoa wa Morogoro na michezo miwili itachezwa na timu za nje ya mkoa huo hapo ili kuweza kuona kasoro na kufanya marekebisho kabla ya kuanza mikimiki ya ligi daraja la kwanza.
0 comments:
Post a Comment