BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

EBOLA SASA YAWAMALIZA MADAKTARI, DAKTARI MWINGINE AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA EBOLA.


Ebola

Ripoti kutoka Sierra Leone zinasema kuwa daktari mwengine amefariki kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Afisa huyo aliambukizwa ugonjwa huo wakati alipokuwa akiwatibu wagonjwa wa Ebola.

Zaidi ya maafisa 20 wa afya wameaga dunia katika taifa hilo huku wengine wengi wakifanya mgomo wakidai marupurupu yao.

Awali ,liberia ili-ufungua mtaa mmoja wa mabanda uliokuwa umetengwa kwa kipindi cha juma moja ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Zaidi ya watu 1500 wamepoteza maisha yao magharibi mwa Afrika kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huo hatari mnamo mwezi Machi.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: