JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA KATIKA KAMATI YA MAUDHUI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA DAR ES SALAAM, SHAURI LA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI NAMBA 5/2014 DHIDI YA CLOUDS TELEVISION UAMUZI WA KAMATI YA MAUDHUI KUHUSU LALAMIKO JUU YA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI, MWAKA 2005.
1.0 Utangulizi:
Tarehe 16/05/2014 na 06/06/2014 kati ya sa 3.00 na 4.00 usiku, kituo cha Clouds Television cha Dar es Salaam kilirusha kipindi cha Bibi Bomba ambacho kilikiuka Kanuni za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005, Kipindi hicho katika tarehe tofauti kilitangaza shindano la kumtafuta mshindi wa bibi bora nchini ambaye angezawadiwa shilingi Milioni kumi.
Maudhui ya kipindi hiki yalidhalilisha mabibi hao washiriki kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na Waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na Kanuni za Huduma ya Utangazaji(Maudhui),2005.
2.0 Maelezo ya kosa
2.1 Kurusha kipindi kinachodhalilisha jamii
Tarehe 16/05/2014 kati ya saa 3.00 usiku na saa 4.00 usiku, Clouds TV walitangaza kipindi cha mahojiano kati ya washiriki wa Bibi Bomba na Waamuzi waliokuwa wakitoa usaili ili kuchuja Bibi bora mmoja ambaye angestahili kupata zawadi hiyo. Maswali yaliyoulizwa yalikuwa ni ya kudhalilisha washiriki hao na wanawake.
Baadhi ya maneno yaliyosikika katika kipindi hicho ni kama yafuatayo:-
2.1.1 Bibi “A”
“Bibi, mara ya mwisho kuhongwa na wanaume ilikuwa lini? Uliwahi kuhongwa mara ngapi? (sikumbuki) kumbe unahongwa sana?,(sijawahi)”;
2.1.2 Bibi “B”
“Bibi, una jicho zuri kama facebook,(asante),una hips nzuri laini kama u-tube,(ndio maana yule Mkerewe akachanganyikiwa)”;
2.1.3 Bibi “C”
“Sema bibiye, swaga zipo? swaga pomoni zimejaa? uko poa weye? King’ast chetu kizima?”;
Akijua kuwa Bibi yule hasikii vizuri, alisema “Bibi, weka Mike sikioni,unasikia vizuri? Weka mdomoni, sasa unasikia vizuri?,”
Bibi aliambiwa acheze na kijana wa kiume (Mwamuzi) mchezo wa kitoto “by show I love you baby”,haya cheza by show I love you baby “
2.1.4 Bibi “D”
Bibi aliambiwa aimbe wimbo na maneno ya wimbo huo ni haya:-
“…..akilala kwangu tumbo lamuuma, akilala kwangu kichwa chamuuma, akilala kwangu kiuno chauma, kwa mke mwenzangu anatetea”
2.1.5 Bibi “E”
Bibi, fish, kachumbali, potatoes, viazi, scrub, uklii, rice uliwahi kula? ”Vegetable uliwahi kula? Beans? chemistry, mathematics uliwahi kula?(sijala)”
2.2 Kutokuwasilisha ratiba ya kipindi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Kituo cha Clouds TV hakikufuata Kanuni za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya kipindi chao kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa ajili ya kuidhinishwa.
Vilevile walitakiwa kutangaza kipindi hicho katika gazeti linalosomwa na watu wengi kabla ya kurushwa hewani.
Kipindi cha Bibi Bomba hakikuwasilishwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wala kutangazwa katika gazeti kabla ya kurushwa. Hii ni kinyume na Kanuni Na. 22(1),(3),(a) na (b).
3.0 Kanuni zilizokiukwa
3.1 Katika kosa la kwanza.
Kituo cha Clouds Television kimekiuka Kanuni Na. 5(b), (c), (d), (f), (g), (h), 14(1), na 15(a), (b) za Huduma ya Utangazaji (Maudhui) 2005, zinasomeka kama ifuatavyo;-
5 Every Licensee shall ensure that the programme and its presentation:-
(b) projects Tanzanian national values and national points of view;
(c ) observes good taste and decency
(d) upholds public morality;
(f) does not injure the reputation of individuals;
(g) protects children from negative influences;
h) does not incite or perpetuate hatred against or vilify, any group or persons on the basis of ethnicity , race, gender, religion or disability.
14(1) Every licensee shall have particular regard to the need to protect children from unsuitable programme material;
15 Every free-to-air licensee shall-
(a) ensure that only official languages, namely Kiswahili and
English are used for all broadcasts except where specific
authorization has been given to use non-official languages;
(b) refrain from using language meant to mislead or unnecessarily
cause alarm and despondency; and.
Tafsiri ya Kanuni hizi kwa mujibu wa Kamati katika shauri hili ni kama ifuatavyo:-
5. Kila mwenye leseni ya utoaji huduma za utangazaji lazima ahakikishe kuwa vipindi vyake vinazingatia:-
(b) kulinda maadili ya Mtanzania na Taifa;
(c ) ubora wa kipindi pamoja na staha;
(d) kuzingatia maadili ya umma;
(f) kutoharibu /kuchafua sifa za watu;
(g) kuwalinda na kuwaepusha watoto kuiga tabia hasi;
h) Kutochochea au kuhamasisha chuki dhidi ya makundi ya watu kwa misingi ya asili, rangi, jinsia, dini au ulemavu.
14(1) Kila mwenye leseni anatakiwa azingatie umuhimu wa kuwalinda watoto na vipindi visivyofaa;
15 Kila mwenye leseni ya utangazaji wa vipindi vya Radio na Televisheni vinavyosikilizwa au kutazamwa bila malipo anatakiwa:-
(a) kuhakikisha lugha pekee zinazotumika katika utangazaji wote ni Kiswahili na Kiingereza isipokuwa pale kibali maalum kinapokuwa kimetolewa kutumia lugha nyingine;
(b) kutotumia lugha ya upotoshaji na yenye kuleta hofu na mfadhaiko.
3.2 Katika kosa la pili
Kituo cha Clouds Television kimekiuka Kanuni Na. 22(1), 22(3)(a), na 22(3)(b) za Huduma ya Utangazaji (Maudhui) 2005, zinasomeka kama ifuatavyo;-
22(1) A licensee shall publish programme schedule in a daily newspaper circulating widely in Tanzania at least one month in advance;
(3) a licensee shall submit to the Authority: –
(a) advance quarterly programme schedule fourteen days before each quarter;
(b) transmission reports detailing programmes actually broadcast within seven days after the end of each calendar month.

22(1) Mwenye leseni anapaswa kuchapisha ratiba ya vipindi vyake katika gazeti linalochapishwa kila siku na kusomwa na sehemu kubwa ya nchi ya Tanzania angalau mwezi mmoja kabla ya vipindi kusikika hewani.
(3) Mwenye leseni anapaswa kuwasilisha kwa Mamlaka :-
(a) ratiba ya vipindi vyake vya robo mwaka siku kumi na nne kabla ya robo mwaka inayotarajia kuanza;
(b) kutoa taarifa za kina za vipindi halisi vinavyotangazwa ndani ya siku saba kabla ya mwisho wa kalenda kila mwezi.
4.0 Ushahidi wa Makosa
4.1 Kuangalia DVD ya kipindi cha Bibi Bomba
Ili kujiridhisha kama maudhui ya kipindi cha Bibi Bomba yalikiuka Kanuni za Utangazaji, Kamati ya Maudhui na uongozi wa Clouds TV waliangalia sehemu zenye makosa ambazo zilikiuka Kanuni za Utangazaji.
5.0 Maelezo ya utetezi
5.1 Maelezo ya Ruge kuomba msamaha kwa jinsi kipindi hicho kilivyofanyika
Mkurugenzi wa Clouds Television Bw. Ruge Mutahaba alianza utetezi wake kwa kusema kuwa ni kweli kituo chake kiliona mapungufu makubwa kwenye vipindi vya Bibi Bomba vilivyorushwa tarehe 16/05/2014 na tarehe 6/06/2014.
Alisisitiza kuwa Uongozi wa Clouds TV ulichukua hatua kali za ndani za kumsimamisha Meneja wa Vipindi pamoja na Mtangazaji wa kipindi hicho aliyejulikana kama Babu na nafasi yake kuchukuliwa na Antonio Nugaz.
Bwana Ruge alisema kwamba shindano hili liliweka mbele utani wa bibi na wajukuu lakini maswali yaliyoulizwa kwenye kipindi cha usaili yalikuwa siyo mazuri na uongozi wa Clouds TV ulikasirika na kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.
Katika suala la washiriki wa Bibi Bomba kutangaza baadhi ya vipindi ya Clouds TV, Bw. Ruge alisisitiza kuwa Clouds TV haikuwa na nia ya kuwaweka mabibi katika nafasi ya utaalamu wa utangazaji kwa masuala yanayohitaji utaalamu wa kuripoti. Huo ulikuwa ni utaratibu wa sehemu ya shindano.
5.2 Maelezo ya Bi. Sakina ambaye ni Mtayarishaji wa kipindi
Mtayarishaji wa kipindi cha Bibi Bomba, Bi. Sakina alitoa utetezi wake kwamba katika kukua kwake amejengwa na taswira ya masihara kati ya bibi pamoja na wajukuu zake na ndio maana kipindi cha Bibi Bomba kina masihara na bibi anatakiwa awe bomba katika kutaniana.
Alisisitiza kwamba kutokana na masihara hayo, tangazaji wa kipindi walikuwa wanamuita mume wao lakini haikuwa na maana ni mume wao kweli.
Bi. Sakina alisisitiza kwamba sehemu ya wimbo katika kipindi cha kwanza ilikuwa ni wimbo kutoka kwa Nyakanga au kungwi katika masuala ya ndoa na kwamba yeye alifika na kuanza kuimba wimbo ule na Clouds TV waliuhariri na kutoa sehemu zisizofaa. Katika kuwachagua hawa mabibi, waliangalia uwezo wao wa kuwaelimisha watu kuhusu mambo mbalimbali ya zamani.
6.0 Kukiri kosa
Mkurugenzi wa Clouds Television alikiri kuwa walifanya kosa la kutangaza kipindi cha kwanza cha Bibi Bomba kwenye msimu wa tatu na kwamba walichukua hatua za kuwasimamisha Meneja vipindi pamoja na Mtangazaji wa kipindi. Yafuatayo ni maneno aliyoyasema;-
“…Kweli walifanya makosa kuruhusu uzembe uliopitiliza katika baadhi ya maswali….”
“…kuna makosa makubwa yalifanyika na tunakubali mbele ya Kamati…lakini sisi ndani yetu kwakuwa tulishayatambua, tuliyachukulia hatua…..”
7.0 Tathmini ya Kamati
Kamati iliridhika kwamba, kituo cha Clouds Television katika kipindi cha Bibi Bomba cha tarehe 16/05/2014 na tarehe 6/06/2014 kilikiuka Kanuni za Utangazaji kwa kutangaza na kuonyesha udhalilishaji kwa washiriki ambao ni mabibi kutokana na maswali ya aibu na kudhalilisha waliyokuwa wakiulizwa na Waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na Kanuni za Huduma ya Utangazaji(Maudhui),2005.
Kamati iliridhika na uamuzi ambao uongozi wa Clouds Television ulichukua kwa kumsimamisha Meneja vipindi pamoja na kumbadilisha mtangazaji wa kipindi baada ya kurushwa kwa kipindi cha kwanza.
8.0 Uamuzi wa Kamati
Kamati iliridhika kuwa kipindi cha Bibi Bomba kilichorushwa tarehe 16/05/2014 na tarehe 6/06/2014 kilikiuka Kanuni za Utangazaji 2005, Na. 5(b),(c),(d),(f),(g);14(1), 15(a),(b) 20(1),(a),(b) na 22(1),(3),(a),(b) kama ilivyonukuliwa hapo juu.
Baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi kutoka kwa Mkurugenzi wa Clouds Television na kwa kuzingatia kuwa wao wenyewe wamekiri kuwepo kwa makosa katika kurusha kipindi cha tangazo hilo na kwamba hatua za nidhamu zimechukuliwa dhidi ya wafanyakazi wao , Kamati ya Maudhui inaamua yafuatayo:-
1.1 Clouds Television inapewa onyo kali;
1.2 Clouds Television inatozwa faini ya shilingi milioni moja za Kitanzania ambazo inapaswa kuzilipa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndani ya mwezi mmoja toka siku ya uamuzi huu.
1.3 Clouds Television wanatakiwa kuwasilisha kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa na kituo chao.
1.4 Clouds Television wawasilishe ratiba za vipindi vyao kwa mujibu wa Sheria.
Endapo Clouds Television itakiuka tena Kanuni za Utangazaji, hatua kali zaidi za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Uamuzi huu umetolewa na kusomwa Dar Es Salaam siku hii ya ….., Mwezi wa Agosti Mwaka 2014.
Haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu iko wazi ndani ya siku 30 tangu uamuzi unapotolewa.
Uamuzi Umesainiwa na:
Eng. Margaret T. Munyagi.
………………………………......
(Sahihi)
Mwenyekiti
WAJUMBE WA KAMATI YA MAUDHUI
1. Bwana Walter Bgoya (Sahihi)..............................................
2. Bwana Joseph Mapunda (Sahihi)........................................
3. Bwana Abdul Ramadhani Ngarawa (Sahihi)………………………..

0 comments:
Post a Comment