BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UGONJWA WA EBOLA YAWAPIGA MKWARA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMA WA TANZANIA KWENDA MAKA KUHIJI KWA MWAKA 2014.


Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum.

Hofu ya ebola huenda ikawanyima nafasi mahujaji Tanzania kwenda kuhiji Maka mwaka huu baada ya raia wa Saud Arabia kufariki kwa ugojwa huo.


Akizungumza na NIPASHE Jumamosi jana, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, alisema kuwa leo, wanatarajia kukutana kuliongelea suala hilo ili kuona kama mahujaji wataenda au la.

Alhadi Salum alisema mpaka sasa baadhi ya mahujaji wameshakata tiketi za kwenda Maka.

“Nipo safarini na jambo hili ni nyeti hasa kutokana na huko tunakoenda tayari mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha kwa ugonjwa huo, tutakaa kwa pamoja kulizungumzia hili, kama safari zitakuwepo au la tutawaeleza,” alisema.

Mwanzoni mwa wiki hii, Wizara ya Afya ya Saudi Arabia ilitangaza kuwa mwathirika wa kwanza wa maradhi ya ebola amefariki dunia nchini humo.

Aidha, kutokana na hofu ya ugonjwa huo ambao huambukiza kwa kasi na kuenea kati ya mtu na mtu kwa kugusa damu na majimaji kutoka kwenye mwili wenye maambukizi, wizara hiyo iliamua watu wote waliokutana na mhanga huyo baada ya kurejea safari ya kikazi nchini Sierra Leone, huwa chini ya uangalizi.

Dalili za ugonjwa huo ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa na vidonda kooni na mara nyingi hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa hutokwa damu ndani na nje ya mwili.

Mara baada ya kutangazwa kujitokeza maradhi ya Ebola katika nchi za Sierra Leone, Liberia na Guinea Conakry, serikali ya Saudi Arabia ilichukua tahadhari za kukabiliana nao kwa kupiga marufuku utoaji viza kwa mahujaji wa nchi hizo.


Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya kesi 1,600 za maradhi hayo zimeripotiwa katika nchi za Sierra Leone, Liberia na Guinea Conacry, ambapo watu zaidi ya 880 wamefariki dunia.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: