BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BIBI WA MIAKA 80 AMNASA VIBAO JAMBAZI NA KUMUUMIZA MDOMONI, ATIMUA MBIO BAADA YA KIPIGO.




Ajuza mwenye umri wa miaka 80 alimpiga mwizi usoni mwake nchini Uingereza na kumuogopesha kiasi cha kutoroka.

Mwanamke huyo, alikuwa anamtembeza Mbwa wake katika mtaa wa Whitstable, Kent, wakati jambazi huyo alipomvamia. Alikuwa amevalia mavazi meusi yaliyokuwa yamefunuika kichwa chake.

Alipigana na jambazi huyo na kumgonga kinywani. Polisi mjini Kent wanasema kuwa wangali wanamsaka jambazi huyo.

Afisaa mkuu wa polisi katika eneo hilo alinukuliwa akisema: ''Inaonekana mshukiwa huyo alimlenga mtu asiye wa kiwango chake.''

Shambulizi hilo lilifanyika wakati wa usiku Afisa mkuu wa polisi pia amewataka wakazi wa eneo hilo kutoa habari kuhusu tukio hilo.

"je unamfahamu mtu yeyote ambaye alikuwa nje wakati wa usiku wakati ajuza huyo alipovamiwa na kurejea nyumbani akiwa na jereha kinywani ?. Tafadhali tunawaomba mtusaidie na uchunguzi wa kisa hiki,'' aliongeza kusema afisaa huyo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: