Na Mtanda Blog, Morogoro.
Chama cha waamuzi mkoa wa Morogoro (Tafca) kimetangaza kutoa mafunzo ya mwisho ya kozi ya awali ya mpira wa miguu na kuwa kozi hiyo imeanza septemba 3 hadi 13 mwaka huu mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu wa chama cha makocha mkoa wa Morogoro, Ahmed Mumba alisema kuwa mafunzo tayari yameanza septemba 3 na yatamalizika septemba 13 mwka huu.
Kozi hiyo ni kozi ya awali ya mpira wa miguu na ndiyo itakuwa ya mwisho kwa mwaka 2014.
Mumba alisema kuwa mpaka sasa tayari chama cha makocha kimetoa mafunzo ya ngazi ya awali na kati kwa kufundisha makocha 97 katika wilaya za Ulanga, Kilombe na Manispaa ya Morogoro.
“Kozi hii itakuwa kozi ya mwisho kwa mwaka huu 2014 kwani mpaka sasa tayari tumefundisha jumla ya walimu wa soka 97 kwa ngazi ya awali 81 na ngazi ya kati 16 hili linatufanya chama kufanya kazi zaidi mwaka 2015 kuhakikisha kunakuwa na walimu wengi wa soka.”alisema Mumba.
Mumba alisema kuwa mwakani chama hicho kitahakikisha kila wilaya inakuwa na walimu wengi waliopta mafunzo ya kozi ya awali ya mpira wa miguu na kati itasaidia vijana wetu wanaelewa mbinu za soka mapema ili baadaye kusaidia taifa sambamba na kujipatia kipato kupitia mpira.

0 comments:
Post a Comment