BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIUNGO MSHAMBULIAJI WA KLABU YA WATFORD AANGUA KILIO BAADA YA KUMFUNGA BAO GOLIKIPA BORA WA DUNIA, NI MANUEL NEUER WA UJERUMANI.


Kiungo wa Klabu ya Watford akimtungua kipa bora duniani

UJERUMANI jana imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Scotland katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Euro, lakini habari kubwa ilikuwa ni Ikechi Anya aliyefunga bao la kufutia machozi dhidi ya mabingwa wa dunia.

Kilio cha furaha: Anya akilia wakati wa kushangilia bao lake jana.


Anya alifunga dakika ya 66 mjini Dortmund ambalo lilikuwa la kusawazisha wakati huo, baada ya Thomas Muller kutangulia kuwafungia wenyeji kabla ya baadaye kufunga la ushindi.


Kiungo huyo wa Watford mwenye umri wa miaka 26, amefurahi mno baada ya kufunga kiasi cha kulia, akisema hakuamini kama ameweza kumfunga kipa bora duniani Manuel Neuer, na akasema hawezi kufanya hivyo kwenye mashindano ya FIFA. .
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: