BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AJALI YASABABISHWA MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA IRINGA KUKOSA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA 2014 IRINGA.

 
PICHA YA MAKTABA IKIONYESHA ASKARI WA HIFADHI YA WANYAMA PORI YA MIKUMI NATIONAL PARK WAKINGALIA SEHEMU YA BASI NDOGO MARA BAADA YA KUPATA AJILI KATIKA HIFADHI HIYO BARABARA KUU YA IRINGA-MOROGORO NA KUSABABISHA WATU 13 KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA WENGENI 13 KUJERUHIWA MKOA WA MOROGORO. PICHA/MTANDA BLOG.

NA FRANK KIBIKI
MWANAFUNZI mmoja wa darasa la saba, katika shule moja wapo manispaa ya Iringa ameshindwa kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba baada ya kupata ajali na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa.


AFISA elimu wa mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, juu ya mtihani huo ulioanza leo chini kote.


Mnyikambi alieleza kuwa tayari wana taarifa za mwanafunzi mmoja ambaye atashindwa kufanya mtihani kutokana  na kulazwa katika hospitali ya mkoa huo akiendelea na matibabu. 


Amewataka wazazi wengine wenye watoto wa darasa la saba ambao hawana tatizo lolote kuhakikiha watoto wao, wanakwenda kufanya mtihani unaoanza leo ili wahitimu elimu ya msingi. 

 
Mkoa wa Iringa, ina zaidi ya wanafunzi 21,540 wanatarajia kufanya mtihani huo katika shule za msingi 458 kati ya 484 zenye wanafunzi wa darasa la saba mkoani Iringa. 


Mnyikambi alisema mpaka sasa amepata taarifa ya mwanafunzi mmoja wa manispaa ya Iringa, ambaye hataweza kufanya mtihani huo baada ya kupata ajali na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Iringa.



Alisema kati ya wanafunzi hao watakaofanya mtihani huo wa darasa la saba, wasichana ni 11,761 na wavulana ni 9,776 huku idadi hiyo ikipungua tofauti na mwaka jana ambapo wanafunzi 23,149. 



Aliwataka wasimamizi wa mitihani hiyo kuzingatia kanuni na sheria kwa kutofanya wizi, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika. 




Kuhusu maandalizi, Mnyikambi alisema mitihani yote imeshawasili wilayani tayari kwa kusambazwa kwenye mashule huku vifaa vingine vikiwa tayari. 

Chanzo http://mwitikio.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: