MAJAMBAZI WAMSULUBU MWALIMU WA KANISA KATOLIKI, MKONO WAKE WAGONGELEA MSUMARI KWENYE MTI NA KUKAA KWA SAA 16 KABLA YA KUOKOLEWA NA POLISI.
Mwalimu wa kanisa Katoliki, Magharibi ya Kenya alijikuta taabani baada ya kutekwa nyara na majambazi waliomtesa pamoja na kumpiga msumari kwenye mti msituni, umbali wa kilomita 200 kutoka nyumbani kwake.
Peter Asutsa alikaa msituni kwa saa 16 mkono wake ukiwa unaning'inia kwenye mti kabla ya kuokolewa na polisi.
Inaarifiwa Peter alipigwa msumari kwenye kwenye mkono wake mmoja baada ya majambazi hao kukosa kumpata na pesa zaidi walizokuwa wakitaka.
Inaarifiwa Asutsa aliizima simu yake na kuificha ndani ya nguo zake za ndani ambapo majambazi hao wasingeweza kuipata.
Baada ya majambazi hao kumtelekeza, alimpigia simu mkewe ambaye aliwaarifu polisi waliokuja kumuokoa.
Masaibu ya Asutsa yalianza pale alipokwenda dukani kumnunulia mkewe mgonjwa dawa katika duka la dawa mjini Kitale Magharibi ya Kenya.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari alimokuwa anasafiria Asutsa aliamrisha dereva kusimamisha gari. Kisha akawafungia ndani akiwa na abiria wengine wawili.
Alitekwa nyara na majambazi waliofika katika sehemu hiyo kwa gari jingine na kumuingiza ndani ya gari hilo na hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa ametekwa nyara.
Walimpora dola 24 na kumtaka asalimu simu yake , lakini akataa.
Baadaye walimpeleka ndani ya msitu na kumpigia msumari mtini kupitia kwenye mkono wake mmoja na kumuacha ndani ya msitu wa Kaptagat.
Alilazimika kuwatisha na kuwafukuza Fisi na Mbweha waliokuwa wakitishia kumvamia usiku.
Aliambia BBC kuwa alihisi maumivu makali.BBC
0 comments:
Post a Comment