BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA POOL NGAZI YA MKOA WA MOROGORO 2014 YAMALIZIKA KWA MANUNG'UNIKO KIBAO.


Na Mtanda Blog, Morogoro.
Mashindano ya mchezo wa pool ngazi ya mkoa wa Morogoro kwa mwaka 2014 yamemalizika mwishoni mwa kwa kupata bingwa mpya na kukabidhiwa zawadi ya sh800,000 huku yakitawaliwa na vurugu zilizojitokeza katika hatua za nusu fainali na fainali ya mashindano hayo mkoani hapa.



Akizungumza na gazeti hili mjini hapa Katibu mkuu wa chama cha pool mkoa wa Morogoro (Mopa) Juma Ng’arare alisema kuwa mashindano ya mwaka 2014 tayari yamepata bingwa wake ambaye ni klabu ya Anathory lakini mashindano hayo yalitawaliwa na vurugu na migomo.

Ng’arare alisema kuwa mashindano hayo yalianza august 29 na kumalizika august 31 mwaka huu lakini vilabu viligombea mashindano kutokana na kutoonekana kwa zawadi wakati yakiwa katika hatua ya nusu fainali na fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika ukumbi wa DDC mjini hapa.

“Haya mashindano yameingia dosari na hii imetokana na chama cha pool taifa kushindwa kumleta mwakilishi wao mapema kutoka makao makuu, kwani jana (juzi) klabu ziligoma kuendelea na mashindano kwa sababu hawajaona zawadi au kiongozi wa chama cha pool taifa hali iliyosababisha vilabu kugomeo michezo ya nusu fainali na kudumu kwa masaa sita.”alisema Ng’arare.

Ng’arare aliongeza kwanza mashindano yalitarajiwa kumalizika majira ya saa 2 usiku lakini kutokana na hali hiyo mashindano yalisimama kwa masaa 6 na kuanza tena saa1:15 usiku na kumalizika saa 8:45 usiku jambo ambalo washiriki hawakutarajia iwe hivyo.

Ng’arare alieleza kuwa majira ya saa 3:30 usiku huo huo ilifumuka vurugu nyingine iliyoanzishwa na vilaku vilivyoshindwa kuendelea na mashindano wakitaka kupatiwa zawadi zao za sh100,000 kama kifuta jasho kutokana na mchanganuo wa utoji zawadi katika mashindano hayo na kulazimika viongozi wa chama cha pool mkoa huo kuomba msaada wa polisi kutuliza hali hiyo.

Vilabu vilivyoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Mzinga, Shan, TPC Masika, Philimon, Mwembesongo, MK Mliti Chamwino na Anathory.



Ng’are alisema kuwa baada ya klabu ya Anathory kuwa bingwa wa mkoa wa Morogoro 2014, klabu ya Philimon ilishika nafasi ya pili na kutwaa zawadi ya sh400,000 huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Shan klabu na kupata sh250,000.

Kwa upande wa wanake mchezaji mmoja mmoja, Rosemary Deus kutoka Mzinga aliibuka ubingwa na kupata sh300,000 wakati Johari Temu wa Anathory alishika nafasi ya pili na zawadi ya sh200,000 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Lilian wa klabu ya Anathory aliyepata sh100,000.

Kwa mchezaji mmoja mmoja wanaume bingwa mtetezi 2013, Mussa Mkwenda alitetea nafasi yake mwaka 2014 kwa kuibuka na ubingwa na zawadi ya sh400,000 huku Juma Kassim akishika nafasi ya pili sh250,000 wote wakitokea klabu ya Anathori. Chanzo Mtanda Blog.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: