BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NENO TUMBILI LAMTOKEA PUANI SHABIKI WA SOKA BRAZIL, AFUKUZWA KAZI NA KUPIGWA MARUFUKU KUONA MECHI ZA SOKA MIAKA MIWILI.


Tumbili akicheza na binadamu.

Mashabiki wa kilabu yasoka ya Gremio nchini Brazil

Mlinda lango mweusi ambaye alibaguliwa kirangi katika mechi moja kubwa nchini Brazil amekataa msamaha kutoka kwa mmoja ya mashabiki waliohusika na kitendo hicho.

Shabiki huyo wa kilabu ya Gremio ,Patricia Moreira amepoteza kazi yake na kutishiwa maisha baada ya kuonekana katika camera akimwita mchezaji huyo wa kilabu ya santos ,Aranha,Tumbili.

Amesema kuwa alitaka kukutana na mchezaji huyo ili kumuomba msamaha binafsi,lakini Aranha amekataa ombi hilo akitaka mashabiki waliohusika na kitendo hicho kuadhibiwa vilivyo.

Bi, Moreira amesema kuwa alilazimika kutoa matamshi hayo ya ubaguzi wa rangi wakati timu yake ilipokuwa ikishindwa katika mechi ya kuwania taji.

Kilabu ya Gremio imepigwa marufuku katika mashindano hayo huku mashabiki ambao watajulikana walitoa matamshi hayo ya kibaguzi wakipigwa marufuku ya kuona mechi za soka kwa miaka miwili.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: