MABINGWA WA KUDHALILISHA WATU KATIKA MITANDAO SASA WAUNDIWA ZENGWE LA NGUVU, SERIKALI YAFICHULIWA SIRI ILI ITOA ADHABU KALI.
Serikali imeshauriwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaotumia vibaya mitandao ili kuondoa vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea kufanyika.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC), Dk. Ayub Rioba, alisema kuwa bado kuna tatizo kubwa la matumizi mabaya ya mtandao na kwamba suala hilo lipo duniani kote.
Dk. Rioba alisema hayo akiunga mkono kauli ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ya kuiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria watumiaji wa mitandao ya kijamii kudhalilisha utu na heshima ya watu.
Lowassa alitoa kauli hiyo juzi kwenye ibada ya mazishi ya mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Lais Metili, aliyefariki wiki iliyopita na picha za mwili wake kusambazwa kwenye mitandao ukiwa hauna nguo.
Dk. Rioba alisema hakuna sheria ya moja kwa moja ya udhibiti wa matumizi mabaya ya mtandao na kwamba jambo hilo bado linafanyiwa kazi, hivyo la msingi ni kuangalia sheria ambazo zinaweza kuwawajibisha wanaotumia mitandao kinyume.
"Zipo sheria ambazo zinaweza kutumika katika kuwashughulikia wanaotumia vibaya mtandao," alisema.
Alisema kuna baadhi ya watu wameonekana kudhalilishwa katika mitandao na wengine hata kutukanwa matusi, hivyo mtu huyo anaweza kuadhibiwa kisheria ili na wengine waweze kuitumia mitandao hiyo vizuri.
"Ipo teknolojia ya kumkamata mtu ambaye ameweka uchafu katika mtandao ama kutumia mtandao vibaya kama mtu anamtukana mwenzeka na ushahidi upo sheria ipo ya kuwajibisha na hawa wanaowazalilisha wenzao katika mtandao wanatakiwa kuwajibishwa kwa kuwa wanafahamika," alisema Dk. Rioba
Dk. Rioba alisema mitandao ikitumiwa vizuri katika jamii inasaidia kuleta maendeleo na kubadilisha uchumi wa watu.
"Kuna mtu mmoja yupo kwenye mtandao huwa anafuga samaki na huwafundisha watu wengine jinsi ya ufugaji huo sasa endapo mtandao ukitumika kinyume itawaumiza wengine," alisema.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
0 comments:
Post a Comment