NYAMA YA BURE !!! GARI LAGONGWA WATU 10 WAKATI WAKIGOMBEA NYAMA YA KIBOKO, WAFARIKI DUNIA.
Nyama ya Kiboko huliwa na watu wengi
Watu kumi walikanyagwa na gari lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation.
Kiboko huyo alikuwa amegongwa na gari na kufariki Jumamosi jioni katika mkoa wa Limpopo wakati ambapo wanakijiji walikimbia katika sehemu hiyo angalau kujipatia kipande cha nyama.
Msemaji wa polisi aliambia shirika la habari la AFP kwamba mnyama huyo aligongwa na wanakijiji wakaona fursa ya nyama ya bure ambapo walikimbia kuinyakua na kuanza kuikatakata, ''
''Hapo ndipo gari lililokuwa linakwenda kwa kasi liliwagonga watu 8 walipokuwa wanakata nyama hiyo na kuwaua,'' aliongeza kusema msemaji huyo wa polisi.
Watu wengine wawili walifariki kutokana na majereha yao mabaya wakiwa wanapokea matibabu hospitalini.
Polisi wanasema kuwa watu wengine saba akiwemo dereva wa gari hilo wanapokea matibabu hospitalini.BBC
0 comments:
Post a Comment