MATUKIO YA AFRIKA.
Mwanamke Mjini Mogadishu.
Shirika la kutetea haki za binaadamu limesema, wanajeshi wa Umoja wa
Afrika wanaolinda amani nchini Somalia wamewadhalilisha kingono
wasichana na wanawake wa kisomali wanaoishi katika mazingira magumu
mjini Mogadishu.
Shirika hilo la Human Rights Watch limesema nchi za kiafrika
zinazochangia wanajeshi hao pamoja na wafadhili wa AMISOM wanapaswa
kushughulikia ukiukaji huo wa haki za binaadamu haraka iwezekanavyo na
kuimarisha uataratibu ndani ya Somalia ya kutafuta haki ya wanawake hao.
Wanawake nchini Somalia
Ripoti hiyo yenye kurasa 71 na iliopewa jina la “‘The Power These Men
Have Over Us' yaani nguvu wanaume hawa walizonazo dhidi yetu, inaonesha
wazi visa walivyofanya wanajeshi hao kwa kutumia misaada ya kibinaadamu
kwa kuwadhalilisha kingono wanawake na wasichana tangu mwaka wa 2013.
Wanajeshi hao wanasemekana kutumia misaada hiyo ili kuwashinikiza wanawake kushiriki vitendo vya ngono.
Ripoti hiyo imeendelea kufafanua kuwa wanajeshi hao waliwabaka baadhi
ya wanawake waliokuwa wakitafuta msaada wa matibabu pamoja na maji
katika kambi za AMISOM.
Kwa mfano mwaka wa 2013 kijana Qamar R
ambalo sio jina lake la kweli aliye na Umri wa miaka 15, alikwenda
katika eneo wanalokaa wanajeshi wa burundi katika kambi ya AMISOM kuomba
usaidizi wa dawa, kwa ajili ya mamake aliyekuwa mgonjwa, baadaye
mkalimani wa kisomali akamuamuru kuwafuata wanajeshi wawili waliokuwa na
dawa hizo, Qamar aliliambia shirika la HRW kwamba badala ya kupewa dawa
alizoitisha alipelekwa katika maeneo ya misitu na kubakwa na mmoja wa
wanajeshi hao, kisha baada ya kitendo akapewa dola kumi na aliyemtendea
unyama huo.
HRW limewahoji wanawake 21 waliopitia masaibu hayo
Aidha shirika hilo la kutetea haki za binaadamu la HRW limekusanya data
zake kwa kuwafanyia mahojiano wanawake 21 na wasichana ambao wameelezea
kubakwa au kudhalilishwa kingono na wanajeshi kutoka Burundi na Uganda
wanaofanyakazi na wanajeshi wa Umoja wa Afrika.
“Baadhi ya
wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanatumia nafasi zao vibaya kwa kuwafanyia
maovu wanawake na wasichana mjini Mogadishu,” alisema Liesl Gerntholtz,
Mkurugenzi wa haki za wanawake katika shirika hilo la HRW.
Nembo ya shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch
Gerntholtz amesema Kwa sasa Somalia ina matatizo mengi lakini Uongozi
wa Somalia na Umoja wa Afrika unaweza kubadilisha hali ilivyo kwa
kuwawajibisha wanajeshi waliotekeleza vitendo vya udhalilishaji wa
kingono.
Miaka mingi ya mapigano na ukosefu wa chakula nchini
Somalia, yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makaazi yao, na bila ya
kazi au kipato chochote cha kumudu maisha, wengi wanategemea usaidizi
kutoka nje na wanalazimika kushawishika katika visa vya udhalilishaji
ili kujikimu kimaisha pamoja na watoto wao.
Itakumbukwa kwamba
mwaka wa 2007 Baraza la usalama la amani la Umoja wa mataifa
liliwapeleka wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia wanaojulikana
kama AMISOM chini ya matakwa ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kulinda miundo mbinu ya Somalia, pamoja na maafisa wa serikali na pia
kusaidia katika kutoa misaada ya kibinaadamu.
AU yaombwa kuingilia kati na kusitisha maovu ndani ya AMISOM
Tangu wakati huo majukumu ya wanajeshi hao pamoja na uwepo wao
uliongezeka maradufu katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika. Wanajeshi wa
AMISOM wanachangiwa na mataifa ya Uganda, Burundi, Kenya, Ethiopia,
Djibouti, na Sierra Leone.
Baadhi ya wanajeshi wa kulinda amani wa AMISOM
Hata hivyo wanaharakati wanasema Umoja wa Afrika hauwezi kulifungia
jicho suala hili maana ya kwamba watakuwa wanaipoteze4a uaminifu umoja
huo katika misheni yake ya kulinda amani Somalia.
Sasa hivi
kinachohitajika ni serikali zinazounga mkono uwepo wa vikosi vya AMISOM
zinapaswa kufanya kazi na Umoja wa Afrika kumaliza visa vya
udhalilishaji wa kingono kwa wasichana na wanawake nchini Somalia na
kuchukua hatua kwa wanajeshi wanaosemekana kutekeleza hujuma hiyo, huku
wakifanya kila wawezalo kusimamisha kabisa visa hivyo.DW
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WANAJESHI WA UMOJA WA AFRIKA WATUHUMIWA KWA KUDHALILISHA KINGONO NA WASICHANA WA KISOMALIA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment