BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SAA ZA GHALAMA KUBWA ZAWATOKEA PUANI MAAFISA WA FIFA WALIZOPEWA KAMA ZAWADI.

FIFA imesema kitendo cha kurejesha saa hizo ni kutunza nidhamu.

Shirikisho la soka la dunia FIFA, limewaambia viongozi wanaounda kamati ya utendaji na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo kurejesha saa zipatazo 65 za gharama walizopokea kama zawadi kipindi cha kuelekea kombe la dunia huko Brazil mwaka huu.
Saa hizo zinakadiriwa kuwa na gharama ya dolla elfu ishirini na tano kila moja na zinatakiwa ziudishwe Octoba 24 ,mwaka huu.

Saa hizo za kumbukumbu ya Parmigiani ziligawiwa na shirikisho la soka la Brazili (CBF) wakati wa mkutano wa maandalizi wa FIFA uliofanyika mjini Sao Paulo.

FIFA imesema kuwa kanuni za maadili zinazuia viongozi kupokea zawadi ambazo zinathamani zaidi au zenye kuonesha ishara fulani.

Inasemekana kwamba saa hizo zitatolewa kwa taasisi zinazojitegemea na si sile zinazojali maslahi huko Brazili.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: