Mwandishi wa gazeti la Habarileo Morogoro, John Nditi akiwa katika harakati za kupata picha za kusalimiana baina ya wachezaji wa netiboli ya Polisi Moro na Zimamoto katika ligi kuu ya netiboli ya muungano ambapo JKT Mbweni waliibuka mabingwa kwa mwaka 2014 yaliyofanyika hivi karibuni uwanja wa jamhuri Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paulo akionyesha vyuma maalumu vinavyotumika katika utekeji wa magari wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa raia mmoja wa Burundi anayetuhumiwa kwa ujambazi.PICHA/MTANDA BLOG
Mchuuzi wa matunda akitembeza matunda aina mbalimbali eneo la kitope kwa kutumi mkokoteni wa baiskeli wakati akisaka wateja wake mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro Anthony Mtaka akifurahia jambo na na Kaimu Mkurugenzi wa mshataka, Anselem Mwampoma kushoto mara baada ya mkuu huyo kufungua mafunzo ya mawakili wa serikali ya uratibu wa shughuli za upelelezi na uendeshaji wa mashauri ya rushwa na udanganyifu yanayofanyika kwa siku tatu mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
Mfanyabiashara wa kebichi Manispaa ya Morogoro, Ruth Mwasongwe akiweka kebichi katika kiroba huku mteja wake akiangalia ambapo kebichi moja huuzwa kati ya sh 300 hadi sh 500 kutokana na ukubwa wake katika soko la Mawenzi mkoani Morogoro, Kebichi hizo hutoka Lushoto mkoa wa Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment