BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TREKTA LAMKONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA KUFARIKI DUNIA KATAVI.

File:Massey Fergusson 6490 Dynashift.JPG
WATU wawili wamekufa kwa kugongwa na trekta katika kijiji cha Mtakata kata ya Magamba wilayani Mlele mkoani Katavi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina mwandamizi msaidizi Dhahiri Kidavashari aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Ramadhan Shaban (20) mwanakijiji wa Kapanda wilaya na Alex Lucas (Makanyanga) mwanakijiji wa Kashaulili mjini Mpanda.

Alisema ajali hiyo ilitokea Septemba 17 mwaka huu saa 2 usiku katika kijiji cha Mtakata wilayani Mlele huku akibainisha kwamba marehemu hao walikuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili T481 CVE aina ya Boxer iliyokuwa ikiendeshwa na Ramadhan wakitoka kijiji cha Kapanga.

Kamanda Kidavashari alisema trekta iliyowagonga ni namba T347 BXV aina ya Tafe lililokuwa likiendeshwa na mtu asiyefahamika huku akibainisha kwamba chanzo cha ajali hiyo ni trekta hilo kuwa na taa moja.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: