BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA KENYA LAILA ODINGA ACHARAZWA VIBOKO KATIKA MKUTANO WA HADHARA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZ_C2jNGyIwlBOLbfrm2mJVxuMoQNr1XIQ4bqCpBs2OLR3SaAFYrvRIGP4Iw7nDozgWWQ-FSFeQbUneup4Lp5a1Qtv0o639Pu5VWL14cayMCOuFkcJ8OAYVQoTrFGVLxAiFY9MJbnKzIk/s1600/photo_1310_large.jpg
Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kumchapa kwa kiboko kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.

Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.

Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga

Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.

Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.

Haijulikani kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wabnasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.

Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: