BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAXIMO KICHEZO, PHILI HALI TETE KWA SARE TANO ZAMPONZA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Marximo-July10-2014.jpg
WAKATI Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo akisema kazi iliyobaki kwa sasa ni kutoa mwito kwa wachezaji wake kuendeleza hali ya kujituma, mwenzake wa Simba, Patrick Phiri anakusudia kuitisha mkutano rasmi kuelezea kwa nini sare zinaendelea kutokea Msimbazi.

Katika mechi za raundi ya tano juzi, Yanga ikiwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, iliwazima wenyeji Stand United kwa mabao 3-0, wakati Simba ikisafiri hadi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ilipata sare ya bao 1—1 na wenyeji wao, Tanzania Prisons.

Katika mchezo wa Yanga, mshambuliaji kutoka Brazil, Geilson Santos maarufu Jaja, alifunga bao la kwanza kutokana na mpira uliogonga mwamba ambao ulipigwa na raia mwenzake wa Brazil, Andrey Continho, kabla ya Jeryson Tegete aliyetokea benchi akimbadili Jaja, kufunga mabao mawili.

Maximo alisema aligundua kuwa wachezaji wake hasa nyota walikuwa hawajitumi inavyotakiwa, lakini kwa sasa ameanza kuona mabadiliko katika kikosi hicho ambacho hiyo ni mechi yake ya kwanza kushinda ugenini msimu huu.

Alisema awali alikatishwa tamaa na kitendo cha timu yake kushinda michezo miwili tu na kutoka sare na Simba na hivyo alikuwa na imani kubwa katika mchezo wa juzi.

Alisema amevutiwa na namna ambavyo hali ya kujituma inavyozidi kuongezeka kwa wachezaji wake hao na kuahidi kuwa atahakikisha kuwa anaendelea kuhamasisha hali hiyo.

“Wachezaji wanatakiwa kuendana na hali ya mchezo, nimefurahishwa na kiwango cha mchezo dhidi ya Stand United na ni imani kuwa kutakuwa na mwendelezo wa ushindi na hali nzuri ya uchezaji,” alisema kocha huyo kutoka Brazil.

Kutokana na ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kwa upande wake, Phiri amesema atafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya timu hiyo.

Sare ya juzi ya bao 1-1 ni ya tano kwa Simba msimu huu katika mechi zake tano, nne zote ikicheza nyumbani. Ina pointi tano ikishika nafasi ya tisa katika msimamo wa timu 14.

Phiri anaonekana kuwa katika wakati mgumu zaidi kwa kuwa ameshindwa kuonesha cheche zake tangu kuanza kwa ligi hasa baada ya mashabiki wa Simba kuwa na imani naye kuwa atairudisha Simba katika chati.

“Kwa sasa sipo katika mazingira mazuri zaidi kuzungumza ila nitafanya hivyo hasa kupitia mkutano rasmi kuelezea mustakabali wa sare hizi na mwenendo mzima wa timu kwa ujumla,” alisema Phiri ambaye ni raia wa Zambia.

Mchezaji Hamisi Maingo wa Tanzania Prison ndiye aliyekatisha furaha ya Simba ya ushindi baada ya kusawazisha bao la Emmanuel Okwi katika dakika ya mwisho ya muda wa kawaida wa mchezo.

Hali hiyo ni mbaya zaidi hasa kwa kuwa Simba wiki hii itakuwa Jamhuri mjini Morogoro kuumana na Mtibwa Sugar ambayo mambo yake msimu huu yameanza vizuri.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: