BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SOKWE MTU WABUNI MBINU MPYA YA KUNYWA MAJI YALIYOTUWAMA KATIKA VIDIMBWI.


Watafiti wamegundua kifaa kipya kinachotumiwa na idadi kubwa ya masokwe.

Wanasema kuwa kifaa hicho ni ishara tosha kwamba masokwe wa mwituni wameanzisha tabia mpya.

Wakati kundi la Watafiti hao lilipokuwa likichukua filamu ya sokwe hao katika kituo kimoja nchini Uganda,walibaini kwamba baadhi yao wamekuwa wakitengeneza sponji la majani ambalo hulitumia kunywa maji.

Tabia hiyo mpya tayari imeanza kuenea kwa sokwe wengine.Mtafiti bingwa Catherine Hobaiter kutoka chuo kikuu cha St.Andrews anasema kuwa sokwe hao huliingiza sponji hilo katika vidimbwi vya maji na baadaye kulifyonza.

Ameiambia BBC kwamba waliona vifaa viwili vipya vinavyotumiwa na sokwe hao.

Anasema kuwa alimuona sokwe mwengine akitumia mmea wa Moss badala ya majani kutengeza sponji lake.

Mwengine alichukua sponji lililotumiwa na mwenzake na kuanza kulitumia.

Amesema kuwa ingawaje habari hizo zinaonekana kama zisizokuwa na maana,masokwe hawajakuwa na tabia kama hiyo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: